Mkurugenzi Mtendaji wa I Hospital ya Benjamin Mkapa (BMH) Dkt. Alphonce Chandika,,akizungumza wakati wa kuelezea mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita ndani ya kipindi cha miaka miwili katika Hospital ya Benjamin Mkapa Dodoma .
Na.Alex Sonna-DODOMA
SEKTA ya Afya imeendelea kuimarika na kuongezeka zaidi Mkoa wa Dodoma katika kipindi cha miaka miwili ya Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwa na miundombinu bora ya Vituo vya kutolea huduma za Afya tofauti na kipindi cha nyuma.
Hayo yamesemwa leo Februari 24,2023 jijini Dodoma na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule wakati akizungumza na waandishi wa habari katika mwendelezo wa Programu maalumu ya kuelezea mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita ndani ya kipindi cha miaka miwili katika Hospital ya Benjamin Mkapa Dodoma .
RC Senyamule amesema kuwa katika kipindi cha miaka miwili chini ya Rais Dkt.Samia huduma ya Afya Mkoa wa Dodoma imeendelea kuwa bora kutokana na kuwepo kwa utoaji huduma bora ambao umekuwa ukitolewa na Hospitali ya Benjamin Mkapa.
”Naipongeza Hospitali ya Benjamin Mkapa kwa kuendelea kutoa huduma mbalimbali kwa wakazi wa Dodoma pamoja na mikoa mingine ambayo imekuwa ikiitengemea Hospitali hiyo ambayo imekuwa ikitoa huduma mbalimbali za Matibabu”amesema RC Senyamule
Amesema kuwa kumekuwa na kituo cha Damu Salama Kanda ya kati kilichopo Mkoani Dodoma, uwepo wa kituo hiki umerahisisha upatikanaji wa damu salama na mazao ya damu.
”Uwepo wa Kituo hicho kimeendelea kusaidia kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi na vifo vya watoto wachanga ikiwa ni pamoja na kupunguza gharama ambazo zilikuwa zinatumika kusafirisha sampuli za damu Kwenda Maabara Kuu ya Taifa iliyopo Dar- es Salaam.”ameeleza RC Senyamule
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa I Hospital ya Benjamin Mkapa (BMH) Dkt. Alphonce Chandika,amesema kuwa wamefanikiwa kupandikiza figo kwa watu 31 na kuokoa fedha kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni 2.3.
Dkt. Chandika amesema katika kipindi cha miaka miwili cha Serikali awamu sita Hospitali ya Benjamin Mkapa imepiga hatua kubwa sana imefanikisha kuimarisha kwa huduma ya upandikizaji wa Figo kwa idadi ya Wagonjwa 31 na kuendelea vizuri na afya zao.
”Tumefanikiwa kuanzisha huduma za upandikizaji wa figo na jumla ya wananchi 31 wamenufaika na huduma hiyo, huku gharama ya huduma hiyo ikiwa ni takriban shilingi milioni 25 wakati India angetibiwa kwa takriban Shilingi milioni 100 ambapo kwa wagonjwa hao 31, Serikali imeokoa zaidi ya Shilingi bilioni 2.3”amesema Dk.Chandika
Dkt.Chandika amesema kwa mwaka 2022/23 hospitali hiyo imeanza ujenzi wa kituo cha mionzi cha matibabu ya saratani ambapo wamepokea Sh.Bilioni 10.
”Serikali inaendelea kutekeleza mrandi mingine katika Hospitali ya Benjamini Mkapa kwa kujenga Jengo la Mionzi Tiba unaogharimu Shillingi Billioni 28 na Serikali imetoa Shillingi 2.9 kwa malipo ya awali kwa Mkandalasi na Ujenzi umefikia asilimia 15.6%.”amesema Chandika