Taasisi ya tiba ya Mifupa na Milango ya fahamu (MOI) imefanya Upasuaji
mkubwa wa Kuondoa Uvimbe kwa kuingia kwenye uvungu wa Ubongo kwa Kutumia
tundu za Pua za Mgonjwa pamoja na kufanya Upasuaji mwingine kwa mgonjwa
aliyekuwa akisumbuliwa na Uvimbe kwenye Uti wa Mgongo.
Upasuaji
huo umefanyika leo Februari 22 Jijini Dar es Salaam kwenye taasisi hiyo
ikiwa ni muendelezo wa mafunzo kwa Vitendo kupitia Kongamano la
Kisayansi la Madaktari Bingwa na Wauguzi wa Ubongo na Milango ya Fahamu.
Akizungumza
mara baada ya Kufanyika kwa Oparesheni hizo Daktari Bingwa wa Upasuaji
wa Ubongo na Milango ya Fahamu Dkt Nicephorus Rutabasibwa amesema
mafanikio ya Upasuaji huo ni matokeo ya Jitihada za Serikali kuipa
kipaumbele Sekta ya Afya kwa Kufanya uwekezaji mkubwa wa Vifaa tiba na
vitendanishi.
“Tumewachagua wagonjwa waliokuwa na matatizo
mbalimbali ambapo mgonjwa wa kwanza alikuwa na uvimbe kwenye kitezi cha
Mgongo ambae dalili zake ilikuwa ni Kichwa kuumwa na baadae alipoteza
kuona, lakini baadae tulipofanya vipimo tukakuta ana uvimbe kwenye
Ubongo ambao unakandamiza mishipa ya fahamu ya kuona” amesema Dkt
Rutabasibwa.
Kwa upande wake Dkt Laurent Mchome ambae pia ni
Mbobezi wa Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya fahamu amesema Upasuaji
uliofanyika leo sio mara ya kwanza Isipokuwa Utalaamu katika Upasuaji
hubadilika mara kwa mara ndio ndio maana wameshirikiana na Wataalamu
kutoka Colorado ili kufanya mafunzo ya pamoja ili kuongeza Ufanisi
katika suala zima la Upasuaji hasa wa kuondoa Uvimbe kwa Wagonjwa
wanaofika MOI kutibiwa.
” Tulianza kwanza kwa kujifunza Darasani
ili tuangalie namna ya kushirikiana katika ujuzi ni mambo yamefika wapi
sasa hivi, kwa sababu inawezekana Binafsi ninasoma na Daktari mwingine
anasoma Binafsi lakini hatukutani pamoja ili kwenda pamoja lakini
mikutano ya namna hii ni muhimu kwa sababu inatukutanisha pamoja
Madaktari na hii inaleta tija zaidi” ameeleza Dkt Mchome
Madaktarii
bingwa wa Ubongo,Mgongo na Mishipa ya fahamu wakifanya upasuaji wa
kuondoa uvimbe kwenye uti wa Mgongo ikiwa ni siku ya tatu ya kongamano
la Kimataifa la Madaktari bingwa wa Ubongo,mgongo na Mishipa
Madaktarii
bingwa wa Ubongo,Mgongo
na Mishipa ya fahamu wakifanya upasuaji wa kuondoa uvimbe kwenye Ubongo
kupitia kwenye pua, ikiwa ni siku ya tatu ya kongamano la Mwaka la
Kimataifa la Madaktari
bingwa wa Ubongo,mgongo na Mishipa likilenga kuwapa Wataalamu hapa
nchini mbinu za kisasa za uchunguzi na matibabu ya uvimbe kwenye Ubongo
na Mgongo ulioambatana na Saratani
Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Ubongo na Milango ya Fahamu Dkt Nicephorus Rutabasibwa alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari leo kuhusu operesheni waliofanya ya upasuaji wa kuondoa uvimbe
kwenye Ubongo kupitia kwenye pua pamoja na Uvimbe kwenye Uti wa Mgongo.
Dkt Laurent Mchome ambae pia ni
Mbobezi wa Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya fahamu akizungumza na
Waandishi wa habari akielezea upasuaji uliofanyika leo kwenye taasisi
hiyo ya MOI na nama utaalamu ulivyotumika kwa kushirikiana na Madaktari
bingwa kutoka sehemu nyingine.