Na Lucas Raphael,Tabora
MAHAKAMA ya wilaya ya Tabora mkonia hapa imemuhukumu mkazi Mmoja wa Ipole katika Wilaya ya Sikonge Mkoani hapa ,Jumanne Kulwa (31) kifungo cha miaka 20 jela baada ya kutiwa hatiani kwa Makosa Manne ya Uhujumu Uchumi .
alisema
Akitoa hukumu hiyo leo Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Tabora , Sigwa Mzige alisema kwamba adhabu hiyo iwefundisho kwa watu wengine wanakiuka maangizo ya serikali ya kuingia kwenye mamlaka ya serikali bila vibali vinavyousika
Alisema kwamba Mshitakiwa alipewa adhabu hiyo ikiwa imebeba Makosa Manne ambayo ni kuingia kwenye hifadhi ,kupatikana na Silaha ,kukutwa na Nyara za Serikali na Silaha za Mlipuko na kujenga kambi .
Alisema kwamba adhabu hiyo ilimetolewa na Mahakama hiyo ambapo Mshitakiwa alitenda Makosa hayo ambayo yamemtia hatiani na kupata adhabu ya kifungo cha Miaka 20 jela, kwani kufanya hivyo ni kwenda kinyume na sheria ya nchi.
Aidha hakimu huyo alisema Mshitakiwa huyo katika kosa la kwanza alitakiwa kulipa faini ya laki 500,000 au kwenda jela mwaka mmoja kosa la pili hadi la nne amehukumiwa kupewa adhabu ya kwenda jela miaka 20 .
“Mahakama hii inazingatia Makosa aliyotenda Mshitakiwa Jumanne Kulwa ya kuhujumu Uchumi ni kosa la kuingia kwenye hifadhi bila ya kuwa na kibali na kukutwa na silaha za moto ,Serikali hairuhusu” Sigwa alisema
Upande wa Wakili wa Serikali Lucy Kyusa aliiambia Mahakama hiyo kuwa Mshitakiwa huyo alitenda Makosa hayo Mnamo 12 April 2022 katika eneo la Isimbila kwenye hifadhi ya Ugalla katika Wilaya ya Sikonge Mkoani Tabora.
Alisema Mshitakiwa Jumanne Kulwa alikamatwa na Maafisa wa wanyamapori kijiji cha Isimbila hifadhi ya Ugalla wilayani humo na alipopekuliwa hakuwa na kibali chochote ambacho kina mruhusu kuingia hifadhini.
Wakitoa ushahidi katika Mahakama hiyo Maafisa wa wanyamapori walisema kwamba walipofanya doria katika hifadhi hiyo kwa kufata nyayo za baiskeli walizifuatilia na kukuta Mshitakiwa akiwa ameweka kambi na waliweza kumkamata hifadhini.
Upande wa utetezi Mashitaka umeweza kuthibitisha Makosa Manne ambapo Mshitakiwa alitenda ikiwemo kujenga kambi katika hifadhi katika kijiji cha Isimbila hifadhi ya Ugalla.
Mshitakiwa Jumanne Kulwa katika utetezi huo alikana kukamatwa ndani ya hifadhini na Maafisa hao kwamba alieleza Mahakama hiyo kuwa yeye hakiwa kwenye hifadhi bali alikuwa anatokea shamba kulima na alikuwa na jembe mkononi mwake.
Baada ya utetezi wake Mshitakiwa aliiomba Mahakama impunguzie adhabu hiyo kwa kuwa ana mke mmoja na watoto wawili ambao wanasoma hivyo Mahakama imuonee huruma kwani anategemewa na Familia yake.