Makamu wa Rais ,Philipo Mpango akizungumza katika mahakama hiyo jijini Arusha.
Makamu wa Rais ,Philipo Mpango akiwa katika picha ya pamoja na majaji mbalimbali katika.mahakama hiyo.
**************************
Julieth Laizer ,Arusha
Arusha. Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano Dk Philip Mpango amesema, Serikali ya Tanzania inatambua umuhimu wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binaadamu na Watu(AFCHPR na itaendelea kufanya nayo kazi .
Hata hivyo, amesema kumekuwepo na changamoto kadhaa katika utekelezwaji wa hukumu za mahakama hiyo na akashauri mahakama kuboresha mahusiano na mahakama za ndani ya nchi, ili kuondoa dhana kuwa mahakama hiyo kuingilia uhuru wa mahakama za ndani.
Amesema ni muhimu kuwepo na ushirikiano na mafunzo baina ya watendaji wa mahakama majaji, Mawakili na mahakimu juu ya masuala ya haki za binaadamu .
Kauli mbiu ya mwaka wa mahakama hiyo mwaka huu ni “kuunganisha mifumo wa sheria za haki za binaadamu za kikanda na kimataifa katika mifumo ya kitaifa”
Rais wa mahakama hiyo, Jaji Imani Aboud akizungumza katika ufunguzi wa mwaka wa mahakama hiyo jijini Arusha , amesema bado nchi nyingi hazitekelezi hukumu za Mahakama hiyo.