Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
HOSPITAL ya Rufaa ya mkoa ya Tumbi, Mkoani Pwani imeanza kutoa huduma ya kusafishwa damu pamoja na mashine za CT-scan pamoja na X-ray za kielektroniki.
Mkuu wa mkoa wa Pwani alhaj Abubakari Kunenge, alieleza neema hiyo kwa wagonjwa na wananchi waliojitokeza hospital ya rufaa ya mkoa ya Tumbi, kupata matibabu ya bure kwa madaktari Bingwa kutoka Hospital ya Muhas Mloganzila pamoja na Hospital ya rufaa ya Tumbi ambao wameshirikiana kutoa huduma za afya bure kwa wanaosumbuliwa na magonjwa mbalimbali ikiwemo sukari,Figo,moyo .
Alieleza kutolewa kwa huduma hizo katika hospital hiyo kunaacha historia ya kero iliyokuwepo kufuata huduma hizo umbali mrefu na hospital nyingine kubwa kama Muhas na Muhimbili.
“Tunashuhudia Serikali ya awamu ya sita ikifanya mageuzi makubwa katika sekta ya afya kwa kusogeza huduma mbalimbali kwa Wananchi ikiwemo vifaa tiba vya aina hiyo,kama x-ray, kuongeza watumishi wa afya ,madawa na kuongeza miundombinu ya vituo vya afya za wilaya “alieleza Kunenge.
“Nimefika kujionea namna huduma hizi zinavyotolewa na kuzungumza na nyie kwa kutambua umuhimu wa kuja kujua hali zenu za kiafya ,ikiwa ni siku ya kwanza ya utoaji wa matibabu hayo kwa siku nne zilizopangwa.”anasema Kunenge.
Mkuu huyo wa mkoa, aliwaasa wananchi, wajenge tabia ya kwenda vituo vya afya, hospital kujua hali zao na kupatiwa matibabu kuliko kusubiri magonjwa yakomae Hali inayosababisha kuchukua muda katika uponaji.
Mkoa wa Pwani una wilaya saba, Halmashauri Tisa, hospital moja ya Tumbi, hospital za wilaya tisa na vituo vya afya 412.