Mkutano
wa Kawaida wa 43 wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC)
unatarajiwa kufanyika jijini Bujumbura, Burundi tarehe 23 Februari 2023.
Mkutano
huo ambao umeanza kwa Ngazi ya Wataalam tarehe19 hadi 20 Februari 2023
utafuatiwa na Mkutano wa Makatibu Wakuu utakaofanyika tarehe 21 na 22 Februari
2023 na kuhitimishwa na Mkutano wa Mawaziri utakaofanyika tarehe 23 Februari
2023.
Mkutano
wa Wataalam utapitia na kujadili agenda mbalimbali muhimu kuhusu masuala ya
mtangamano wa Jumuiya hiyo ambazo baadaye zitawasilishwa kwenye Mkutano wa ngazi ya
Makatibu Wakuu utakaofanyika tarehe 21 na 22 Februari 2023 kwa majadiliano na
hatimaye agenda hizo zitawasilishwa kwenye Mkutano ngazi ya Mawaziri
unaotarajiwa kufanyika jijini hapa tarehe 23 Februari 2023.
Miongoni
mwa agenda hizo ni pamoja na Taarifa ya Utekelezaji wa maazimio yaliyofikiwa
kwenye vikao vilivyopita katika maeneo mbalimbali ikiwemo biashara na forodha,
miundombinu, ulinzi na usalama, sheria, utalii, ajira na utawala na fedha; Kupokea
taarifa ya mwaka ya Ukaguzi wa Hesabu za Jumuiya kwa mwaka wa fedha ulioishia
mwezi Juni 2022; Taarifa ya Ofisi ya Katibu Mkuu wa Jumuiya; Taarifa kuhusu Taasisi za Jumuiya ya Afrika Mashariki pamoja
na kupitia na kupitisha ratiba ya shughuli za Jumuiya kwa kipindi cha kuanzia
mwezi Januari hadi Juni 2023.
Ujumbe
wa Tanzania kwenye Mkutano wa Ngazi ya Wataalam unaongozwa na Mkurugenzi wa
Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki, Balozi Stephen Mbundi. Ujumbe huo pia unajumuisha
Wajumbe kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Wizara ya
Ujenzi na Uchukuzi, Wizara ya Fedha na Mipango na Wizara ya Katiba na Sheria.
Kadhalika Mkutano huo
umehudhuriwa na Wajumbe kutoka nchi zote wanachama ambazo ni Burundi ambaye ni mwenyeji wa mkutano, Kenya, Uganda, Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Sudan Kusini ambao wameshiriki kwa
njia ya mtandao.
Kiongozi wa Ujumbe wa Rwanda akishiriki Mkutano wa Wataalam |
Ujumbe wa Uganda ukishiriki Mkutano huo |
Ujumbe wa Kenya nao ukiwa katika Mkutano |
Kiongozi wa Ujumbe wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo nae akishiriki mkutano wa wataalam |
Wajumbe kutoka Taasisi za Jumuiya ya Afrika wakishiriki mkutano wamaandalizi ya mkutano wa 43 wa Baraza la Mawaziri wa EAC |
Wajumbe kutoka Sekreatarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki wakishiriki Mkutano wa Wataalam jijini Bujumbura |
Mkurugenzi wa Uendelezaji wa Sera, Ofisi ya Rais, Menejementi ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi Agnes Meena akishiriki Mkutano wa Wataalam |
Mkurugenzi wa Biashara, Uwekezaji na Sekta za Uzalishaji katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Bernard Haule akishiriki mkutano wa wataalam |
Sehemu nyingine ya ujumbe wa Tanzania wakishiriki Mkutano wa Wataalam |
Sehemu ya Wajumbe wa Sekretarieti ya EAC wakifuatilia mkutano |
Mkutano ukiendelea |
Wajumbe kutoka Tanzania katika mkutano |
Mkutano ukiendelea |