NAIBU Waziri wa Afya Dk. Godwin Mollel ,akizungumza wakati akifungua Mkutano wa Mwaka wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri $ Lishe na Afya ya Uzazi na Mtoto ulioanza leo Februari 20 hadi Februari 22 jijini Dodoma.
KATIBU Mkuu Wizara ya Afya Prof Abel Makubi,akizungumza wakati wa Mkutano wa Mwaka wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri $ Lishe na Afya ya Uzazi na Mtoto ulioanza leo Februari 20 hadi Februari 22 jijini Dodoma.
NAIBU Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(OR-TAMISEMI) anayeshughukia afya Dkt. Grace Magembe ,akizungumza wakati wa Mkutano wa Mwaka wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri $ Lishe na Afya ya Uzazi na Mtoto ulioanza leo Februari 20 hadi Februari 22 jijini Dodoma.
SEHEMU ya Washiriki wakifatilia hotuba ya Naibu Waziri wa Afya Dk. Godwin Mollel (hayupo pichani) wakati akifungua Mkutano wa Mwaka wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri $ Lishe na Afya ya Uzazi na Mtoto ulioanza leo Februari 20 hadi Februari 22 jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe Ofisi ya Rais TAMISEMI Dr.Ntuli Angelile Kapologwe,akizungumza wakati wa Mkutano wa Mwaka wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri $ Lishe na Afya ya Uzazi na Mtoto ulioanza leo Februari 20 hadi Februari 22 jijini Dodoma.
MWENYEKITI wa Waganga Wakuu wa Mikoa Tanzania Dkt. Best Magoma,akizungumza wakati wa Mkutano wa Mwaka wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri $ Lishe na Afya ya Uzazi na Mtoto ulioanza leo Februari 20 hadi Februari 22 jijini Dodoma.
Na.Alex Sonna-DODOMA
NAIBU Waziri wa Afya Dk. Godwin Mollel amesema kuna haja ya kuandaa na kutengeneza mfumo mmoja wa kidigitali utakaounganisha huduma za afya zote nchini ili kuwezesha ufanisi wa kiutendaji katika sekta ya afya.
Hayo ameyasema wakati akifungua Mkutano wa Mwaka wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri $ Lishe na Afya ya Uzazi na Mtoto ulioanza leo Februari 20 hadi Februari 22 jijini Dodoma.
Dk. Mollel amesema kuwa kuna haja ya kutengeneza mfumo mmoja wa kidigitali utakaounganisha huduma za afya nchini.
“Tuna mifumo mingi ambayo wakati mwingine inachanganya na inatushinda kutumia, niwaombe maafisa TEHAMA wa Wizara ya Afya na OR-TAMISEMI watutengenezee mfumo mmoja ili tupunguze mikanganyiko ya mifumo hii mingi” amesema Dk.Mollel
“Tunatakiwa kuwa na mfumo mmoja ambao kipimo cha CT-Scan kikifanyika Mtwara mtu wa makao makuu ataona, dawa zikitolewa Kigoma zitaonekana kwenye mfumo, hii itatusaidia kufanya kazi kwa ufanisi lakini pia itatuondolea mkanganyiko na kuzuia upotevu wa dawa na vifaa tiba” ameongeza
Aidha Dk. Mollel amemtaka Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa ya Taifa (MSD) kuhakikisha kuwa anapeleka vifaa tiba na dawa mahospitalini ndani ya saa 24 baada ya kupokea fedha kutoka serikali kuu ili kuboresha hali ya utoaji na upatikanaji huduma za afya.
Dk. Mollel amesema kuwa ili kuboresha huduma za afya ni lazima kuwepo kwa dawa na vifaa tiba vya kutosha katika maeneo ya kutolea huduma.
“Mkurugenzi uko hapa na umesikia, kuna wakati hospitali zina fedha zao mkononi lakni MSD hana dawa ila kwenye maduka ya dawa ya watu binafsi dawa zipo, Serikali imefanya kazi kubwa sana ya ujenzi wa miundombinu lakini vituo vingi havifanyi kazi kwa sababu ya ukosefu wa vifaa tiba na dawa, tukitoka hapa MSD mliangalie hili vizuri na kuhakikisha baada ya malipo dawa zinatolewa ndani ya saa 24” amesema Dk. Mollel.
Akijibu pia hoja ya kuwepo kwa changamoto ya gharama kubwa za matibabu zinazowashinda wagonjwa kumudu Naibu Waziri Dk. Mollel alisema kuwa dawa pekee ya kukabiliana na changamoto ya gharama za matibabu kwa wananchi ni kupitishwa kwa sheria ya Bima ya Afya kwa Wote.
Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Afya Prof. Abel Makubi amesema kuwa ni vyema mifumo ya kimtandao ikapunguzwa kupitia eGa ikabaki mifumo michache itakayoweza kuwasiliana ili kurahisisha utendaji kazi na uboreshwaji wa huduma za afya nchini.
Awali akisoma hotuba ya Waganga Wakuu, Mwenyekiti wa Waganga wakuu wa Mikoa (RMO’s) Dk. Best Magoma amesema kuwa mpaka kufikia mwezi Januari mwaka huu tayari serikali imeipelekea MSD Bilioni 129 tsh/- sawa na asilimia 68 ya bajeti ya mwaka wa fedha 2022/2013 ambayo ni Bilioni 200 kwa ajili ya ununuzi wa Dawa na vifaa tiba.