NAIBU Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Mhandisi Kundo Mathew,akimkabidhi Tuzo ya Heshima Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe.Rosemary Senyamule iliyotolewa na Klabu ya Waandishi wa habari Mkoa wa Dodoma kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan kwa kutambua mchango wake katikka Tasnia ya Habari wakati wa tamasha la usiku wa Habari Dodoma lililoandaliwa na Klabu ya Waandishi wa habari Mkoa wa Dodoma (CPC) .
MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Mhe.Rosemary Senyamule,akizungumza wakati wa tamasha la usiku wa Habari Dodoma lililoandaliwa na Klabu ya Waandishi wa habari Mkoa wa Dodoma (CPC) lililofanyika jijini Dodoma.
MWENYEKITI wa Klabu ya Waandishi wa habari Mkoa wa Dodoma Bw.Mussa Yusuph,akizungumza wakati wa tamasha la usiku wa Habari Dodoma lililoandaliwa na Klabu ya Waandishi wa habari Mkoa wa Dodoma (CPC) lililofanyika jijini Dodoma.
MWENYEKITI wa Kamati ya Maandalizi Bi.Sakina Abdulmasoud,akielezea lengo la tamasha hilo wakati wa tamasha la usiku wa Habari Dodoma lililoandaliwa na Klabu ya Waandishi wa habari Mkoa wa Dodoma (CPC) lililofanyika jijini Dodoma.
MKURUGENZI Mtendaji wa WazoHuru Media Bw.Mathias Canal,akizungumza wakati wa tamasha la usiku wa Habari Dodoma lililoandaliwa na Klabu ya Waandishi wa habari Mkoa wa Dodoma (CPC) lililofanyika jijini Dodoma.
NAIBU Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Mhandisi Kundo Mathew,akiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa habari Mkoa wa Dodoma mara baada ya kufungua tamasha la usiku wa Habari Dodoma lililoandaliwa na Klabu ya Waandishi wa habari Mkoa wa Dodoma (CPC) na kuhudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe.Rosemary Senyamule,Viongozi wa Vyama vya Siasa, waandishi wa Habari wa mkoa huo na wadau mbalimbali wa sekta hiyo lililofanyika jijini Dodoma.
PICHA ZOTE NA ALEX SONNA
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Dodoma (CPC), kimetoa tuzo ya heshima kwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kutokana na dhamira yake ya kuhakikisha uhuru wa vyombo vya habari unaimarika na kuanza kushughulikia vikwazo vinavyoikabili sekta ya habari nchini.
Tuzo hiyo imetolewa katika hafla ya usiku wa waandishi wa habari mkoani Dodoma iliyoandaliwa na CPC kwa udhamini wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji(EWURA), Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na taasisi ya Wazo Huru na mgeni rasmi wa hafla hiyo alikuwa Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Kundo Mathew.
Akitoa maelezo ya tuzo hiyo iliyopokelewa kwa niaba na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule ambaye ni Mlezi wa chama hicho, Mwenyekiti wa kamati ya utoaji tuzo, Nelly Mtema, amesema Rais Samia alipoingia madarakani aliagiza kufunguliwa kwa vyombo vya habari vilivyokuwa vimefungwa na kuanzishwa kwa mchakato wa mabadiliko ya Sheria ya Huduma za Habari nchini ya mwaka 2016 iliyokuwa ikilalamikiwa na wadau kwenye baadhi ya vipengele.
“Pia katika uongozi wa Rais Samia amefanikisha kubadilishwa kwa viwango vya ada za usajili wa channel za mtandaoni ambapo kwasasa ni Sh.500,000 badala ya Sh.Milioni moja, hatua hii imewezesha waandishi wengi chipukizi kujiajiri kwa kufungua channel hizo,”amesema.
Kuhusu uchumi wa vyombo vya habari na waandishi wa habari, Mtema amesema kupitia Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, imeundwa kamati maalum ya kuchunguza hali ya kiuchumi kwa vyombo vya habari na waandishi wa habari ili kunusuru uchumi wa sekta hiyo.
Aidha, amesema tuzo ya kiongozi bora wa kitaifa kwa mwaka 2022, imetolewa kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Dkt.Selemani Jafo kutokana na kuwa kiongozi anayezingatia muda katika utekelezaji wa majukumu yake hasa yanayohusisha waandishi wa habari.
Katika hafla hiyo, CPC ilitoa tuzo ya kutambua mchango wa Wizara Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kwenye tasnia ya habari iliyopokelewa na Naibu Waziri Kundo huku Mkuu wa Mkoa Senyamule akipewa tuzo ya kutambua ushirikiano anaowapa waandishi wa habari wa Dodoma kwenye utekelezaji wa majukumu yao.
Pia, tuzo ya mwandishi bora wa habari Mkoa wa Dodoma kwa mwaka 2022 alishinda Augusta Njoji kutoka gazeti la Nipashe, Afisa Habari bora ilikwenda kwa Nteghejwa Hosea kutoka Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Mwanachama bora wa CPC ilikwenda kwa Jackline Victor na tuzo ya Mwandishi Chipukizi ilitolewa kwa Rasul Kidindi.