Na Alex Sonna-FULLSHANGWE BLOG
WAWAKILISHI Katika Michuano ya Klabu Bingwa barani Afrika Timu ya Simba SC imeshindwa kutamba katika uwanja wa nyumbani baada ya kuzamishwa bao 3-0 na Raja Casablanca kutoka nchini Morocco Mchezo wa Kundi C uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
Bao la wageni lilifungwa mnamo dakika ya 30 na Hamza Khabba baada ya kuwazidi maarifa mabeki na viungo wa Simba na kuachia shuti kali lililomshindwa Aishi Manula.
Kipindi cha pili timu zote zilifanya mabadiliko hata hivyo wageni walifaidika na mabadiliko hayo kwani waliweza kupata mabao mawili kupitia kwa Soufiane Benjdid dakika ya 82 na Ismael Mokadem dakika ya 85 kwa Mkwaju wa Penalti
Kwa ushindi huo Raja Casablanca imeweka rekodi ya kupata Pointi tatu katika uwanja wa Taifa kwani Simba tangu 2013 haijawahi kufungwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa.
Kwa matokeo hayo Kundi C Raja Casabblanca amefikisha Pointi 6,nafasi ya pili Horoya wenye Pointi 4,Vipers pointi 1 wakiwa nafasi ya tatu huku Simba akishika nafasi ya nne akiwa hana pointi wala bao.