Na Victor Masangu,Pwani
Kinyang’anyiro cha kumsaka mlimbwende wa miss Pwani kinatarajiwa kufanyika aprili 28 mwaka huu Wilayani Kibaha kwa kushirikisha mabinti wa fani ya urembo kutoka Wilaya mbali mbali.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari mjini Kibaha kuhusiana na Maandalizi ya shindano hilo Mkurugenzi mtendaji wa Twiga Entertainment Ireen almaarufu (Twiga) amesema kwa hatua za awali za Maandalizi zimeshaanza kufanyika.
Twiga alisema kwamba shindano la mwaka huu litakuwa la aina yake ukilinganisha na msimu uliopita kutokana na kuongeza ubunifu zaidi katika mambo mbali mbali ili liweze kuvutia zaidi kwa wadau wa urembo.
“Kwa sasa tumeshaanza hatua za awali za maandalizi ya kuelekea shindano la kumsala mlimbwende wa Mkoa wa Pwani na nina amini safari hii Mambo yatakwenda vizuri zaidi ya msimu uliopita wa mwaka 2021 kwa hiyo wadau wakae mkao wa kupata burudani,”alisema Twiga.
Aidha Mkurugenzi huyo alibainisha kuwa zoezi la uchukuaji wa fomu kwa ajili ya ushiriki wa shindano limeshaanza kufanyika katika maeneo mbali mbali ya Wilayani Kibaha na kwamba mwisho wa kurudisha fomu itakuwa aprili 12.
Pia alifafanua kuwa baada ya kumalizika kwa hatua ya kurudisha fomu hizo kutafanyika usahili aprili 15 kwa warembo wote ambao watakuwa wamejitokeza katika kuwania taji la miss Pwani.
Katika hatua nyingine aliwaomba wadau wa fani ya urembo wakiwemo makampu i binafsi pamoja na wawekezaji wa mkoa wa Pwani pamoja mashirika ya umma kujitokeza kwa hali na mali katika kudhamini shindano hilo lengo ikiwa ni kuwapa fursa warembo kuonyesha vipaji vyao ili waweze kutimiza ndoto zao.
Twiga Entertainment imekuwa mstari wa mbele katika kushiriki katika shughuli mbali mbali za kijamii pamoja na kukuza vipaji katika sekta ya michezo burudani pamoja na fani ya ulimbwende.
Kampuni hiyo mnamo mwaka 2021 ulifanikiwa kwa kiwango kikubwa baada ya kuaanda miss pwani kwa mara ya kwanza na kufanikiwa kupata warembo ambao waliweza kuipeperusha vema bendera ya Mkoa wa Pwani.