Kiasi cha shilingi milioni 74.5 kutoka fedha za maendeleo ya mfuko wa Jimbo la Ilemela zimetumika kwaajili ya ujenzi wa barabara ya kutoka Igombe senta kuelekea mwaloni kwa kiwango cha Zege
Akizungumza wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo ndani ya Jimbo la Ilemela Mbunge wa Jimbo hilo Mhe Dkt Angeline Mabula amesema kuwa kiasi hicho cha fedha kimetumika kumaliza kero ya muda mrefu iliyokuwa ikiwakabili wananchi na wafanya biashara wa eneo hilo Ili waweze kuendelea na shughuli zao za kiuchumi na kijamii
‘… Tumshukuru sana Rais Dkt Samia Suluhu Hasan ametoa fedha Ili tukamilishe barabara muendelee na shughuli zenu, na hivi karibu tutaanza pia ujenzi wa chuo cha VETA kati ya vile 63 vya nchi nzima, tumpongeze sana ..’ alisema
Kwa upande wake mwakilishi wa Meneja wa wakala wa barabara za mijini na vijijini TARULA Bwana Gavidas Mlyoka amesema kuwa kiasi hicho cha fedha kimetumika kujenga mita 180 kati ya mita 320 za urefu wa barabara yote na kwamba utekelezaji wa mradi huo unaendelea vizuri
Nae mkurugenzi wa manispaa ya Ilemela Mhandisi Modest Apolinary ameahidi kutoa kiasi cha shilingi milioni 63 kutoka fedha za mapato ya ndani kumalizia kiasi cha mita 140 kilichobaki ili wananchi wa eneo hilo waweze kunufaika na mradi huo
Akihitimisha Katibu wa CCM wilaya ya Ilemela Bi Aziza Isimbula amesema kuwa utekelezaji wa mradi huo ni ufanikishaji wa Ilani ya uchaguzi ya chama chake Kwa wananchi mara baada ya wananchi kukiamini chama hicho wakati wa uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka 2020 hivyo kuomba waendelee kuwaunga mkono na kumshukuru Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais Dkt Samia Suluhu Hasan
Mbunge wa Jimbo la Ilemela Dkt Angeline Mabula yupo jimboni kwaajili ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo, kupokea ushauri,pongezi na kusikiliza kero na changamoto za wananchi wake