Mkurugenzi wa Muungano wa Klabu za waandishi wa habari Tanzani (UTPC) Kenneth Simbaya akizungumza na waandishi wa habari kwenye mafunzo ya uandishi wa habari za maudhui mbalimbali (MULTI-CONTENT JOURNALISM)
Mkuu wa kitengo cha habari Ubalozi wa Marekani Michael Pryor akizungumza wakati wa kufungua mafunzo ya kuwajengea uelewa waandishi wa habari wa kuandika habari za maudhui mbalimbali
Waandishi wa habari wakiwa kwenye mafunzo ya uandishi wa habari za maudhui mbalimbali (MULTI-CONTENT JOURNALISM)
Mohammed Mvumbagu msaidizi wa masuala ya habari mtandao na maudhui (wakwanza kulia)akiwafunduisha baadhi ya waandishi wa habari moja kati ya program zinazotumika katika kutengeza habari (Inshot) waliohudhuria mafunzo ya uandishi wa habari za maudhui mbalimbali
************************
Na Hellen Mtereko, Mwanza
Muungano wa Klabu za waandishi wa habari Tanzania (UTPC) kwakushirikiana na ubalozi wa Marekani (U.S.EMBASSY) wametoa mafunzo ya uandishi wa habari za maudhui mbalimbali (MULT-CONTENT JOURNALISM) kwa waandishi wa habari 15 Jijini Mwanza.
Mafunzo hayo ya siku moja yamefanyika katika ukumbi wa Adden Palace uliopo Wilaya ya Ilemela Mkoani hapa.
Akizungumza wakati wa kufungua mafunzo hayo Mkuu wa kitengo cha habari Ubalozi wa Marekani Michael Pryor, amesema mafunzo hayo yatawasaidia waandishi wa habari kutumia dhana zao muhimu katika kutekeleza majukumu yao ya kuhabarisha jamii.
Amesema waandishi wa habari wakiyatumia vizuri mafunzo hayo yatakuwa chachu ya kuchochea utendaji kazi katika ulimwengu wa kidigitali.
Kwa upande wake Mtaalamu wa mambo ya habari kutoka Ubalozi wa Marekani Japhet Sanga, amewakumbusha waandishi wa habari kufuata Sheria,taratibu na kanuni za uandishi kabla ya kupeleka habari kwenye jamii hatua itakayosaidia kuepukana na migogoro isiyo ya lazima.
Awali akizungumza kwenye mafunzo hayo Mkurugenzi wa Muungano wa Klabu za waandishi wa habari Tanzania (UTPC) Kenneth Simbaya, amesema mafunzo hayo yanalenga kuwaongezea ujuzi waandishi wa habari ili wafanye kazi zenye ubora zitakazoongeza thamani ya tasnia hiyo kwenye jamii.