Mkuu wa Idara ya Kitengo cha Mionzi na Picha katika Hospitali ya Mkoa wa Tanga Bombo,Dkt Goodluck Mbwilo akizungumza kuhusu uwekezaji huo mkubwa uliofanywa na Rais Dkt Samia Suluhu kwa ajili ya ujenzi wa jengo na ununuzi wa Mashine ya CT scan ambao umesaidia kwa asilimia kubwa kuwapunguzia mzigo wananchi waliokuwa wakifuata huduma hiyo mikoa mengine, kulia ni Mteknolojia Mionzi katika Hospitali hiyo, Bw. Athumani Rajabu
Mashine ya CT Scan inayotumika katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga- Bombo
Mteknolojia Mionzi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo Bw. Athumani Rajabu akizungumza wakati akionyesha mashine kubwa waliyoipata yenye uwezo mkubwa wa kufanya uchunguzi kwa wagonjwa zaidi ya 100 kwa siku na Serikali imefanya kama zawadi kwa wananchi wa mkoa wa Tanga.
Mteknolojia Mionzi katika Hospitali ya Mkoa wa Tanga Bombo Bw. Athumani Rajabu, akifanya matayarisho ya awali kabla ya kuwahudumia wagonjwa wanaohitaji kipimo cha CT Scan
Na Oscar Assenga,Bombo- Tanga.
SERIKALI ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu umeweka historia kubwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo baada ya kufanya uwekezaji wa kiasi cha zaidi ya Bilioni 2 zilizotokana na miradi ya Uviko 19 kwa ajili ya ujenzi wa jengo na ununuzi wa Mashine ya CT Scan ambao umesaidia kwa asilimia kubwa kuwapunguzia mzigo wananchi waliokuwa wakifuata huduma hiyo mikoa mengine.
Akizungumza leo Mkuu wa Idara ya Kitendo cha Mionzi na Picha katika Hospitali hiyo Dkt Goodluck Mbwilo alisema kwamba wanaishukuru Serikali kwa uwekezaji huo mkubwa ambao umeandika historia kwa mkoa huo ambapo awali hawakuwahi kuwa na mashine kama hiyo kutokana na kwamba mashine hizo zilikuwa zikipatikana kwenye hospitali za Rufaa za Kanda na Taifa.
Alisema kwenye hospitali hizo ndio zilikuwa zikipatikana lakini kwa sasa kila hospitali ya mkoa kupitia Rais Dkt Samia ameweza kufanikisha hilo na hiyo itasaidia kutoa huduma bora kwa watanzania wakiwemo wagonjwa wa ajali na wenye matatizo ambao wanahitaji huduma ya CT Scan kwa ajili ya uchunguzi.
Aidha alisema kwamba awali wagonjwa walikuwa wakipata rufaa kwenda katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili au Hospitali ya Rufaa ya KCMC ambako huko napo gharama zilikuwa ni kubwa sana hivyo kwa sasa huduma hiyo inapatikana kwenye hospitali ya Bombo hivyo wananchi wachangamkie fursa hiyo kwa kuweza kupata matibabu na kuokoa gharama kubwa ambazo awali walikuwa wakizitumia.
“Kwa kweli tunaishukuru Serikali ya awamu yaa Sita kwa uwekezaji huu mkubwa ambao awali haukuwepo haya ni mapinduzi makubwa kwenye sekta ya afya kwa mkoa wetu hivyo niwaombe wananchi watumie fursa hiyo kujitokeza kuweza kuja kupata vipimo”Alisema
Hata hivyo alisema kwa sababu gharama za vipimo zipo chini ukilinganisha na hospitali binafasi huku akiwashauri watanzania hususani wakazi wa Mkoa wa Tanga na mikoa mengine kuchangamkia mpango wa fursa ya kuwa na bima ya afya ili kuwarahisishia kupata huduma za matibabu pindi wanapokuwa wakiugua.
Awali akizungumza Mteknolojia Mionzi katika Hospitali hiyo, Athumani Rajabu alisema mashine kubwa waliyoipata ina uwezo mkubwa inaweza kufanya uchunguzi kwa wagonjwa zaidi ya 100 kwa siku na Serikali imefanya kama zawadi kwa wananchi wa mkoa wa Tanga.
Alisema mara nyingi wagonjwa ambao wanapata ajali hususani za barabarani na magonjwa ambayo hayaambukizi kama Saratani ,Kiharusi wanapopata wagonjwa wa nama hiyo kipindi cha nyuma walikuwa wanashindwaa kujua yupi ana madhara zaidi au atapata unafuu zaidi hivyo wote walikuwa wanapatiwa Rufaa kwenda Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na hali inapokuwa ikijitokeza wanapofika Muhimbili na kufanyiwa vipimo vya CT Scan wengine wanagundulika wana matatizo kidogo ambao wangeweza kupona kwenye hospitali walizotoka.
Athumani alisema kwamba hiyo mashine imeweza kupunguza gharama kwa wananchi zisizo za lazima ambao wamekuwa na uhitaji wa huduma za matibabu za upasuaji wa kichwa hivyo uwekezaji huo mkubwa uliofanywa na Serikali umetoa kama msaada kwa sababu ya ghamara zinazotolewa zipo chini
mfano ukienda sehemu za pembezoni,kandokando huduma ya Ct Scan imekuwa ikichangiwa na wagonjwa hadi laki nne hadi tatu na nusu.
Hata hivyo alisema kwamba mradi huo uliofanywa na Serikali wananchi watatibiwa kwa gharama nafuu za laki na nusu kwa waagonjwa ambao hawatawekewa dawa na laki mbili na arobaini ambao watawewekewa dawa ukiangalia gharama hizo na zile zinazotozwa kwenye hospitali zengine ni kama utaona ni msaada ambao serikali imeamua kutoa kwa wananchi,
Athumani alisema awali hospitali hiyo haijawahi kuwa na na daktari bingwa wa mionzi lakini kwa sasa wamepata madaktari ambao wapo kwenye hospitali hiyo na wanashauku ya kuweza kuwahudumia wananchi wa mkoa wa Tanga huku akieleza kwamba kuna huduma nyengine za Ct Scan zimeongezeka na huduma za utrsa sound kuangalia mishipa ya damu kwa watu wanaovimba miguuu ikiwemo kuangalia ubongo wa watoto wadogo