MKURUGENZI Mtendaji wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB) Asangye Bangu akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) ,wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali za bodi hiyo leo Februari 15,2023,jijini Dodoma.
IMEELEZWA tangu kuanzishwa kwa mfumo wa stakabadhi za Ghala mwaka 2007, zaidi ya kilo bilioni 2.3 za mazao mbalimbali zimekusanywa katika maeneo mbalimbali nchini.
Aidha amesema kuwa mafanikio yaliyopatikana baada ya kuanzishwa kwa mfumo wa Stakabadhi za Ghala ni pamoja na ongezeko bei la za mazao, mapato ya mkulima na mapato ya serikali kwa wastani wa asilimia 200 kutokana na urasimishaji.
“Mafanikio mengine ni ongezeko la uzalishaji wa mazao kwa wastani wa asilimia 12 kwa mwaka, mfumo huu pia ni kichocheo cha ubora wa mazao yanayofikishwa sokoni, upatikanaji wa takwimu sahihi za mazao yanayopita kwenye mfumo wa Stakabadhi za Ghala, ongezeko la mapato ya
uhakika kwa serikali kuu na serikali za mitaa, kukuza huduma za fedha vijijini, kufanikisha uanzishaji wa soko la bidhaa Tanzania”ameeleza
Hata hivyo Bw.Bangu ametoa wito kwa madalali kuacha tabia ya kuwarubuni wakulima na badala yake kuwaacha waingie kwenye mfumo wa Stakabadhi ghalani ili kuuza mazao yao kulingana na bei iliyopo sokoni.
“Natoa wito kwa madalali waache kuwarubuni wakulima wawaache wajiunge katika Mfumo wa Stakabadhi ghalani ili waweze kuuza mazao yao kwa bei ya ushindani iliyopo sokoni kwa kuendelea kuuza mazao shambani inaendelea kuwadidimiza wakulima kwa sababu madalali wengi wananunua mazao kwa bei ya chini tofauti kabisa na bei iliyopo kwenye mfumo,”amesema Bangu