NJOMBE
Halmashauri ya wilaya ya Njombe imefanikiwa kujenga kituo Cha afya Cha kisasa kupitia Mapato ya ndani katika kata ya Mwango ambapo katika mradi huo majengo mbalimbali yatayokuwa yakitoa huduma tofauti kwa wagonjwa yamejengwa .
Awali wakazi wa kata ya Mtwango walikuwa wakilazimika kufata huduma katika hospitali ya Kibena mjini Njombe huku wengine wakienda katika hospitali binafsi ya Ikelu ambayo wengi wao walikuwa wakishindwa kumudu gharama za matibabu jambo ambalo limekuwa ni muarobani kwao kwasasa .
Miomgoni mwa majengo yaliyojengwa katika kituo hiki kwa kutumia fedha za makusanyo ya Mapato ya ndani ni jengo la wagonjwa wa nje(OPD) ,Jengo la wagonjwa wa Ndani( IPD),Jengo la Baba, Mama na mtoto(RCH),Jengo la mihonzi (x-ray), Jengo la upasuaji, Jengo la akina mama wajawazito,Jengo la kuhifadhi maiti pamoja na Jengo la maabara.
Katika kuokoa Maisha ya watu Halmashauri hiyo inaendelea na uboreshaji wa huduma za afya katika maeneo mengine ikiwa ni pamoja na ujenzi wa Zahanati na vituo vya afya.