Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya uchukuzi na biashara Iringa LTD, Caroline Mwakabungu akizungumza na waandishi wa habari juzi ofisini kwake kumuomba Rais Samia Suluhu Hassan kuwasaidi kupata hati ya kampuni hiyo ilichukuliwa mwaka 2019 na Tume ya uchunguzi wa mali za serikali wakati wa serikali ya awamu ya tano.PICHA PAUL MABEJA
Na Paul Mabeja,IRINGA
MKURUGENZI mtendaji wa kampuni ya uchukuzi na biashara Iringa LTD, Caroline Mwakabungu amemuomba Rais Samia Suluhu Hassan kuwasaidi kupata hati ya kampuni hiyo ilichukuliwa mwaka 2019 na Tume ya uchunguzi wa mali za serikali wakati wa serikali ya awamu ya tano.
Mwakabunge, alitoa ombi jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu usumbufu pamoja na manyanayaso ambayo wamekuwa wakiyapata kutoka kwa wanasiasa na mamlaka mbalimbali za kiserikali.
Alisema anamuomba Rais Samia kumsadia kupata hati hiyo ambayo ilichukuliwa mikono mwa marehemu baba yake Dk. Lucas Mwakabungu, aliyekuwa mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi kwa madai kuwa wanakwenda kuikagua.
“Mwaka 2019 walikuja watu kutoka Tume ya uchunguzi mali za serikali iliyoundwa wakati wa utawala wa hayati Rais Magufuli na kampuni hii kabla ilikuwa mali ya serikali ikijulikana kama RETCO,lakini mzee wangu na wenzake walinunua wakati ule wa sera ya ubinafsishaji chini ya uongozi wa Rais Mkapa.
“Walipokuja wakadai kuwa wao ni tume ya serikali ambayo inakagua mali za serikali kama ziliuzwa kihali baba alijaribu kugoma kutoa hati ile lakini walimwambia kama anakataa watampa kesi ya uhujumu uchumi ikabidi aitoe lakini hadi leo hatujui ipo wapi kwani tumeenda hadi Hazina wanadai hawajui ilipo”alisema Mwakabungu
Vilevile, alisema kutokana na hali hiyo hawajui nini hatima yao kwakua kuchukuliwa kwa hati kumekuwa ndiyo chanzo cha wao kupata usumbufu na vitisho kutoka kwa baadhi ya viongoi wa serikali kutaka waondoke katika kampuni hiyo kinyume cha utaratibu.
“Mimi ni mtoto wa marehemu nilichaguliwa kama mkurugenzi mtendaji na mwanahisa ninae wakilisha hisa nyingi na ninae wakilisha kundi la watu wenye hisa nyingi kwenye kampuni nimekuwa nipipata misukosuko mingi kutoka kwa watu mbalimbali kinyume na sheria ya makampuni binafsi.
“Hata hivi ninavyozungumza na nyinyi hapa ninayo barua ya mkuu wa mkoa ambayo inanitaka nikabidhi ofisi ndani ya saa 48 kwa kamati ambayo sijui hata imeundwa na nani na jambo la ajabu ni kwamba hii ni kampuni binafsi inakuaje mamlaka za serikali zinaingilia kinyume na sheria ya kampuni binafsi kuna siri gani nyuma ya pazia”alihoji
Kadhalika, alisema anamuomba Rais Samia kuingilia kati mgogoro huo kwakua unakatisha tamaa kwa wawekezaji wazawa kinyume na jitihada zake ambazo amekuwa akizifanya kuweka mazingira wezeshi hasa kwa wanawake.
Pia, alisema kuchukuliwa kwa hati hiyo kumesababisha mambo mengi kukwama ikiwemo kushindwa kupata mikopo kwenye taasisi za fedha ili kufanya uwekezaji.
“Tunafanya kazi tukiwa hatujui nini hatma ya kampuni hii kwani toka kupokonywa hati imekuwa domant (haiendelei) kwakuwa tunashindwa hata kuingia ubia na wawekezaji wengine,kukopa fedha hivyo kukosesha mtaji wa kujiendesha na kuikosesha mapato serikali”alisema
Naye, Mwanasheria wa kampuni hiyo Mpeli Mwabungu alisema wanaiomba serikali kuingilia kati sakata hilo kutokana na uwepo wa tabia ya baadhi ya viongozi kuingilia maamuzi kwa kutoa matamuko ya kisiasa ambayo yanasababisha baadhi ya wapangaji wao kugoma kulipa kodi kwa madai kuwa hilo ni eneo la serikali.