Wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Ufundi Tanga (Tanga School) wakiendelea na ubunifu wa Incuber aambacho ni maalumu kwa ajili ya kutotoleshea mayai ya kuku kupitia katika mradi mafunzo ya ubunifu na ujasiriamali ambayo yanaendelea shuleni hapo kupitia Taasisi ya Tanzania Open Innovation Organization (TOIO) yenye Makazi yake Jijini Tanga na Dar chini ya fadhilwa na Shirika la Foundation Botnar ambao wamelenga kuhakikisha Vijana wanajifunza masuala mbalimbali ya ubunifu ili kuweza kujikwamua kiuchumi.
Mwazilishi wa Taasisi ya Tanzania Open Innovation Organization (TOIO) yenye Makazi yake Jijini Tanga na Dar,Shaukatali Hussein akionyesha waandishi wa habari ambao hawapo pichani pikipiki waliobuni inayotumia umeme
Wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Ufundi Tanga (Tanga School) wakiangalia pikipiki inayotumia umeme iliyobuniwa kupitia mradi mafunzo ya ubunifu na ujasiriamali ambayo yanaendelea shuleni hapo kupitia Taasisi ya Tanzania Open Innovation Organization (TOIO) yenye Makazi yake Jijini Tanga na Dar chini ya fadhilwa na Shirika la Foundation Botnar ambao wamelenga kuhakikisha Vijana wanajifunza masuala mbalimbali ya ubunifu ili kuweza kujikwamua kiuchumi.
Wanafunzi wakiendelea kupata elimu
Mwazilishi wa Taasisi ya Tanzania Open Innovation Organization (TOIO) yenye Makazi yake Jijini Tanga na Dar,Shaukatali Hussein akitazama vitu mbalimbali vilivyobuniwa na wanafunzi wa shule hiyo
Na Oscar Assenga,TANGA
VIJANA Jijini Tanga wameshauriwa kuchangamkia fursa ya mafunzo mbalimbali ya ubunifu na ujasiriamali yanayotolewa katika maeneo yao ili kuweza kuwasaidia kuwa wajasiriamali wakubwa hatua itakayowawezesha kujiingizia kipato na kuweza kujikwamua kiuchumi wao na jamii zao.
Wito huo ulitolewa na Mwazilishi wa Taasisi ya Tanzania Open Innovation Organization (TOIO) yenye Makazi yake Jijini Tanga na Dar,Shaukatali Hussein wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mradi mafunzo ya ubunifu na ujasiriamali ambayo yanaendelea kwenye shule ya Sekondari Tanga School.
Mafunzo hayo yanaendeshwa na Taasisi hiyo chini ya fadhilwa na Shirika la Foundation Botnar ambao wamelenga kuhakikisha Vijana wanajifunza masuala mbalimbali ya ubunifu ili kuweza kujikwamua kiuchumi.
Alisema kwamba ubunifu ndio silaha pekee ambayo inaweza kuwainu vijana kiuchumi uwepo wataizingatia kwa umakini na kujituma hasa kutokana na utandawazi hivyo wanapaswa kuchangamkia fursa mbalimbali zinazotolewa.
” Dunia ya sasa ubunifu umekuwa muhimu kwa jambo lolote ambalo linafanywa hivyo niwahimize vijana kuona umuhimu wa kuchangamkia fursa zilizopo kwenye maeneo yenu hususani miradi inayoanzishwa” Alisema.
Aidha alisema Taasisi hiyo imejikita kuhakikisha inafanya kazi ya kuhamasisha vijana kuchangamkia fursa mbalimbali ikiwemo kwenye sekta ya Kilimo,Afya, Elimu, Pikipiki za umeme, taa za sola na Ubunifu kwa kuwapatia vijana mafunzo.
“Katika mradi huu tumepanga kuwafikia vijana 900 kwa kata zote 27 za Jiji la Tanga na mpaka sasa vijana tumewafikia vijana 170 na tunaamini tutawafikia wote hivyo nitoe wito kwa wazazi na walezi kuwahimiza vijana wao kuchangamkia fursa hii”Alisema.
Hata hivyo alisema mafunzo wanayopatiwa vijana hao ni katika fursa za Kilimo,Afya na teknolojia mbalimbali Jinsi ya kuunda na kutengeneza vitu mbalimbali na pia mafunzo hayo yanapatikana bila gharama yoyote
Awali akizungumza mmoja wa wanafunzi wanapata mafunzo hayo Sedrick Samweli anayesoma kidato cha nne alisema Mambo wanayofundishwa ya ubunifu yatakuwa chachu kubwa kwao kuwa wabunifu wakubwa ndani na nje ya nchini hapo baadae.
“Kwani hapa tunafundishwa vitu mbalimbali vya ubunifu ambavyo vinatuandaa katika maisha ya baadae ikiwemo namna ya kutengeneza Incubator ambayo inatumika kutotolesha mayai ya aina yoyote hivyo inatusaidia kupanua wigo mpana” Alisema.
Hata hivyo alisema pia wamekuwa na mradi wa kutumia mtandao kuwasaidia wagonjwa kuwasiliana na madaktari Hospitalini hatua ambayo inapunguza muda wa mgonjwa kufika na kumkosa na kurudi hivyo kumuondolea usumbufu.
Pia alisema kwamba mradi huo umekuwa chachu kwao kwani wamekuwa wakijifunza pia namna ya kutengeneza baiskeli na pikipiki za kutumia umeme ambazo zitaweza kuja kuisaidia jamii siku zijazo.