Mkaguzi msaidi kutoka Trafiki Makao Makuu dawati la elimu Faustina Ndunguru akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutoa elimu kwa madereva katika eneo la daraja la watembea kwa miguu katika Wilaya ya Ilemela Jijini Mwanza.
Sajenti Jeremiah Makoromu kutoka Polisi Trafiki Wilaya ya Nyamagana dawati la elimu( kushoto) akivuka kwenye Kivuko na watembea kwa miguu
Wakwanza kulia ni Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Mkoa wa Mwanza Sunday Ibrahimu wakijadiliana jambo na Mkaguzi msaidizi kutoka Trafiki Makao Makuu dawati la elimu Faustina Ndunguru (kushoto)
Mkuu wa Kikosi Cha Usalama Barabarani Mkoa wa Mwanza Sunday Ibrahimu (wapili kulia) akishuka kwenye dalaja la watembea kwa miguu namadeva pikipiki baada ya kuwapatia elimu
*******************************
Na Hellen Mtereko, Mwanza
Maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani Kitaifa yatafanyika katika Mkoa wa Mwanza Machi 13 hadi 17 mwaka huu, wananchi wote wanao miliki vyombo vya moto wameombwa kupeleka vyombo vyao ili vifanyiwe ukaguzi na kupatiwa stika ambayo itakuwa ni uthibitisho kwamba vyombo hivyo vimefanyiwa ukaguzi.
Hayo yamebainishwa jana Ijumamosi Feburuari 11, 2023 na Mkuu wa Kikosi Cha Usalama Barabarani Mkoa wa Mwanza Sunday Ibrahimu, wakati akitoa elimu kwa madereva Bajaji,Pikiki,Dalala, wananchi wanaotumia vyombo vya moto na watembea kwa miguu katika Wilaya ya Nyamagana na Ilemela.
Amesema lengo la kutoa elimu kwa makundi hayo ni kuwajengea uelewa wa matumizi sahihi ya barabara ambao utawasaidia kupunguza ajali zisizo za lazima.
Ibrahimu amesema kauli mbiu ya mwaka huu ni “Tanzania bila ajali inawezekana timiza wajibu wako” ambapo ameeleza kila mmoja akitimiza wajibu wake nchi itaendelea kuwa salama.
Kwaupande wake Mkaguzi msaidizi kutoka Trafiki Makao Makuu dawati la elimu Faustina Ndunguru, amewasisitiza madereva kuzingatia sheria,taratibu na kanuni za usalama barabarani ili kuepuka ajali zinazochangia kuangamiza maisha ya watu huku wengine wakiachwa na ulemavu wa kudumu.
Amesema wataendelea kutoa elimu kwa makundi mbalimbali ya madereva Mkoani humo ili wawe salama wao pamoja na abiria wanaowabeba na atakaekwenda kinyume na utaratibu watamuajibisha kisheria.
Naye Sajenti Jeremiah Makoromu kutoka Polisi Trafiki Wilaya ya Nyamagana dawati la elimu, amewakumbusha watembea kwa miguu wanapofika kweye Kivuko wachukue tahadhari kubwa sana kabla ya kuvuka ikiwemo kubonyeza swichi ya taa ili ibadilike kutoka nyekundu kuwa ya kijani baada ya hapo wajilizishe kwa kuangalia kulia,kushoto na kulia ili wavuke kwa usalama.
Madereva waliopewa elimu wamelihakikishia Jeshi la Polisi kutoa ushirikiano kwa kuwaripoti wenzao wanaokiuka Sheria za usalama barabarani hatua itakayosaidia kufanya kazi zao kwa weledi.