Naibu katibu mkuu wa machinga Taifa Joseph Mwanakijiji akiongea na waandishi wa habari mkoani Iringa juu ya kulaani vurugu zilizotokea jijini Mwanza Jana.
Na Fredy Mgunda, Iringa.
SHIRIKISHO la Umoja wa Machinga Taifa (SHIUMA) limelaani vitendo vya vurugu vikivyofanywa na wafanyabiashara wadogo wadogo Jana jijini Mwanza kwa kusababisha hasara kwa baadhi ya wafanyabiashara wakubwa na wananchi wengine.
Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Iringa,Naibu katibu mkuu wa machinga Taifa Joseph Mwanakijiji alisema kuwa wanalaani vikali uvunjifu wa amani ulitokea jijini Mwanza ulisababishwa na mgambo kuchukua hatua mkononi bila kufuata sheria walizojiwekea baina ya serikali na shirikisho hilo.
Mwanakijiji alisema kuwa wamekuwa wanafanya mazungumzo ya mara kwa mara na serikali juu ya namna bora ya kutafuta maeneo rafiki na wafanyabiashara wadogo wadogo lakini bado serikali imekuwa ikiwapangia wafanyabiashara hao maeneo ya mbali ambayo sio rafiki na biashara hiyo.
“Sisi kama Viongozi wa Taifa wa kundi hili la Machinga tunalaani vikali sana, uvunjifu uliofanyika Mwanza, maana sisi siyo wanaharakati wa kuhamasisha fujo, isipokuwa ni taasisi inayoshughulikia mambo yote kupitia meza za mazungumzo bila kuchoka”alisema mwanakijiji
Mwanakijiji alisema kuwa jana wameona kwenye mitandao ya kijamii au kwenye vyombo mbalimbali vya habari kuwa , wafanyabiashara wakubwa wa maduka Mwanza,Wilaya ya Nyamagana, walifunga maduka baada ya Vurugu ambazo zilitokana na mgambo kuchukua bidha za machinga kwa kutumia nguvu.
“Moja ya taarifa zinazosambaa sana ni kwamba maduka yaliibiwa bidhaa na magari kufanyiwa fujo kadhaa wa kadhaa,ikumbukwe Mwanza wapo watoto wa mitaani wengi Sana (uzurulaji) na kunawakati inapelekea kwenye mchangamano na wengine wanakuwa hawana nia njema, na inawezekana iyo imepelekea uvuninjifu kwa kiasi na kiwango kikubwa”alisema mwanakijiji
Alisema kuwa shirikisho hilo haliamini kuwa machinga ndio waliovunja maduka na magari na kuiba vitu vya watu,machinga wanabiashara zao na hawawezi kuwa wezi huo ni uzushi tu.
Mwanakijiji alisema kuwa machinga wanamahusiano mazuri na wafanyabiashara wakubwa kuanzia ngazi ya juu hadi huku chini hivyo hawawezi kuwavunjia na kuwaibia wafanyabiashara wenzao,wizi huo umefanywa na baadhi ya watoto wa mtaani.
“Sisi Machinga na wafanyabiashara wakubwa, tuna mahusiano mazuri na makubwa sana, hasa kama viongozi Taifa na hata wasaidizi wetu tumewambia mara zote kwenye vikao vyetu vya Taifa wanaotoka kwenye Mikoa yote Tanzania na ieleweke kuwa wafanyabiashara na sisi tunategemeana kwa kiasi kikubwa sana”alisema mwanakijiji
Mwanakijiji alisema kuwa shirikisho linatoa Pole kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana kwa tatizo lilotokea na wamewaomba Machinga wote wa mwanza kuwa watulivu katika kipindi ambacho wanalitafutia ufumbuzi Jambo hilo.
Alimazia kwa kusema kuwa wanampongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan Kwa namna anavyoendelea kuwashika mkono kwa kuhakikisha wanaimalika kiuchumi siku hadi siku
Itakumbukwa akiwa Geita kwenye ziara alitoa maelekezo Kwa wakuu wa Mikoa yote Tanzania kutoa kiwanja kwajili ya ujezi wa ofisi za Machinga kila Mkoa na pesa za ujezi alishatoa kiasi Cha shillingi million mia mbili na sitini 260,000,000 ambazo ni sawa na shillingi million kumi kila Mkoa 10,000,000=. Vile vile Billion arobaini na Tano 45,000,000,000 kama bajeti kupitia Bunge Kwa kundi hili na millioni mia Saba (700,000,000 za Iringa