Mkuu wa mkoa wa Arusha,John Mongela akizungumza katika uzinduzi wa kituo hicho jijini Arusha.
Katibu mkuu wa jumuiya ya Afrika Mashariki,Peter Mathuki akizungumza katika uzinduzi huo jijini Arusha.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Makongoro Nyerere akizungumza katika uzinduzi wa kituo hicho.
……………………………..
Julieth Laizer,Arusha.
Arusha.Mkuu wa mkoa wa Arusha ,John Mongela amewataka vijana kukitumia kituo cha amani na utafiti cha Hayati Mwalimu Julius Nyerere kilichopo makao makuu ya jumuiya ya Afrika Mashariki kujifunza na kuyaenzi yale yote yaliyoanzishwa na Nyerere.
Mongela ameyasema hayo leo jijini Arusha wakati akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki,Dk Stergomena Tax wakati akizundua rasmi kituo hicho ambacho kilikuwepo tangu mwaka 2006 .
Mongela amesema kuwa,Hayati Mwalimu Julius Nyerere alijipanga sana kuhakikisha anadumisha amani uchumi na maendeleo katika nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki huku akihakikisha analinda na kutetea amani barani Afrika.
Mongella ameongeza kuwa, Hayati mwalimu Nyerere alikuwa ni muumini wa amani na umoja bara Afrika na ndio sababu aliweza kuongoza kamati kadhaa ikiwepo ya ulinzi na amani ya Afrika.
Kituo hicho kilichopo katika Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki kitaendeshwa na Jumuiya hiyo kwa ushirikiano na chuo kikuu Cha Arcadia Cha Marekani na Taasisi ya American Graduate school ya nchini Ufaransa.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo,Dk Peter Mathuki amesema EAC itaendelea kuenzi jitihada za hayati Mwalimu Nyerere katika kuimarisha amani na umoja barani Afrika.
“Leo tunawapa Ubalozi viongozi Hawa kama ishara ya kuendelea kutuamini mchango wa mwalimu Nyerere katika kulinda amani na lengo la kituo hicho ni kuwaandaa vijana wa Afrika ya Mashariki katika masuala ya amani “amesema
Amesema kupitia Kituo hicho vijana watapata udhamini wa kusoma masuala ya amani na lengo miaka kikiwezesha chuo Kituo hicho kuwa chuo kikuu .
Dk Mathuki amesema hayati Nyerere katika maisha yake alikuwa akisisitiza amani na umoja kwa bara zima la Afrika na alifanya kazi kubwa ambayo mafanikio yake hadi sasa yanaonekana.
Amesema kuwa, wakati EAC inatarajiwa kuongeza wanachama ikiwepo nchi za Somalia suala ya amani ni moja ya mambo muhimu kwatka Jumuiya hiyo ambayo itakuwa na watu zaidi ya million 300.
Wakizungumza katika uzinduzi huo,Makongoro Nyerere na Joseph Butiku ambaye alikuwa Katibu wa Nyerere, wamesema uzinduzi wa kitabu hicho ni ishara kuwa bado EAC inamuenzi mwalimu Nyerere.
Makongoro amesema kuwa, yeye kama mtoto wa Nyerere na familia yake wanashukuru EAC kuendelea kumuenzi vizuri mwalimu Julius Nyerere na Kituo hicho kitasaidia sana vijana kujiendeleza katika masuala ya amani.
Kwa upande wake Butiku alishukuru Jumuiya ya EAC kumuenzi mwalimu Nyerere na kuendelea kutambua mchango wake katika masuala ya amani ,umoja na utulivu barani Afrika.
Butiku ameshukuru EAC kuwapa Ubalozi wa heshma wa EAC Yeye, Makongoro na aliyekuwa msaidizi binafsi wa mwalimu Nyerere Samweli Kasori .
Awali Profesa Warren Haffar wa chuo kikuu cha Arcadia amesema watashirikiana na EAC katika kuhakikisha Kituo hicho kinasaidia vijana kusoma na kufanya utafiti juu ya masuala la amani.
Jumuiya ya Afrika ya Mashariki hadi Sasa Ina nchi Saba ambazo ni Kenya, Uganda,Tanzania, Rwanda, Burundi, Sudani Kusini, Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo na hivi karibuni nchi ya Somalia inatarajiwa kupokelewa.