Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yahaya Nawanda akizungumza wakati wa Kikao cha Tathmini ya Utekelezaji Mkataba wa Lishe, Chanjo na Bima ya Afya kwa Wote kilichohudhuriwa na wadau mbalimbali wa afya.
Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yahaya Nawanda ameagiza kila Halmashauri ya wilaya Mkoani Shinyanga kuhakikisha inafikia asilimia 100 ya chanjo ya kuzuia saratani ya mlango wa kizazi kwa wasichana wa umri wa miaka 14 (HPV) dozi ya kwanza (HPV 1) ifikapo Machi 15,2023 na asilimia 100 kwa HPV dozi ya pili ifikapo Septemba 2023.
Dkt. Nawanda ametoa agizo hilo leo Alhamisi Februari 9,2023 wakati wa Kikao cha Tathmini ya Utekelezaji Mkataba wa Lishe, Chanjo na Bima ya Afya kwa Wote kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa afya.
Lengo la Kikao hicho ni kufanya tathmini ya utekelezaji wa Mkataba wa Lishe kwa kipindi cha Mwezi Julai hadi Desemba 2022 uliosainiwa baina ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan na Wakuu wa Mikoa yote ya Tanzania bara Septemba 30,2022.
Wadau wakiwa ukumbini.
Licha ya kuwapongeza watoa huduma kwa kufikia asilimia 100 ya utoaji wa chanjo ya UVIKO – 19 , Polio na chanjo ya kuzuia donda koo, Dkt. Nawanda amesema Chanjo ya kuzuia saratani ya mlango wa kizazi kwa wasichana wa umri wa miaka 14 (HPV) na Chanjo ya Surua si ya kuridhisha hivyo kuagiza Halmashauri kuchukua hatua kufikia malengo yaliyokusudiwa.
“Naelekeza kila halmashauri ihakikishe inafikia asilimia 100 ya chanjo ya HPV dozi ya kwanza (HPV 1) ifikapo Machi 15,2023 na asilimia 100 kwa HPV dozi ya pili ifikapo Septemba 2023. Pia kila halmashauri ihakikishe Chanjo ya Surua Rubella dozi ya pili iwe imefikia kiwango cha asilimia 100 ifikapo Septemba 15,2023”,amesema Dkt. Nawanda.
Akizungumzia kuhusu Utoajia Huduma za Lishe, Nawanda amesema Mkoa wa Shinyanga unaendelea kutekeleza afua za lishe ambapo umetekeleza kwa ufanisi mkubwa kwa baadhi ya viashiria vilivyo kwenye mkataba wa Lishe. Lakini takwimu zinaonyesha viashiria vya utoaji wa fedha zilizopangwa kutekeleza shughuli za lishe, utoaji wa huduma za chakula kwa wanafunzi shuleni, upimaji madini joto kwenye chumvi bado hauridhishi.
“Halmashauri zilizotoa fedha kwa kiasi kidogo zaidi ni Manispaa ya Shinyanga (34.66%), Msalala (43.89%), na Ushetu (48.46%), hivyo nawaelekeza Wakurugenzi kuhakikisha fedha zilizopangwa kutekeleza afua za lishe zinatolewa zote kabla ya Juni 30,2023. Pia Halmashauri za Kishapu na Ushetu kuhakikisha vitendanishi vya kupimia uwepo wa madini joto (Lodine test kit) kwenye chumvi vinakuwepo na upimaji ufanyike”,amesema Dkt. Nawanda.
Wakurugenzi wa Halmashauri na wadau wa afya wakiwa ukumbini.
Pia amewataka Maafisa Elimu (Msingi na Sekondari) na Wakuu wa Shule washirikiane na kamati za shule kuhakikisha chakula kinatolewa kwa wanafunzi kulingana na mwongozo wa lishe shuleni.
Kuhusu Bima ya Afya kwa Wote, Dkt. Nawanda amesema bima hiyo itasaidia kutatua changamoto za huduma ya afya hivyo kuwataka viongozi wa ngazi mbalimbali kuhakikisha wanahamasisha wananchi kupata huduma ya bima ya afya kwa wote pindi Mswada utakapopitishwa Bungeni.
Katika hatua nyingine amewataka Wakuu wa wilaya na Wakurugenzi kushirikiana na watoa huduma za afya ili kuhakikisha huduma za afya zinatolewa kwa ubora unaostahili huku akiwataka pia Wakuu hao wa Wilaya kuhamasisha wananchi kupata Vyeti vya kuzaliwa ndani ya siku 90 baada ya kuzaliwa ambavyo vinatolewa bure.
“Vyeti vya kuzaliwa vitolewe ndani ya siku 90 na iwe ajenda kwenye vikao vya Baraza la Madiwani. Hamasisheni wananchi wanapata vyeti vya kuzaliwa kwa haraka ili watoto wawe na vyeti ili kuepuka safari za kwenda kwa Wakuu wa wilaya kufuatilia vyeti vya kuzaliwa. Tuachane na tabia ya kufuatilia vyeti vya kuzaliwa watoto wakiwa na umri wa miaka 16”,amesema Mkuu huyo wa Mkoa.
Katika kikao hicho cha tathmini, wadau wamejadiliana kwa kina sababu za baadhi ya viashiria kutotekelezwa kama ilivyotarajiwa na kuweka mikakati thabiti ya kuongeza kasi ya utekelezaji wa kuinia hali ya lishe mkoani Shinyanga. Kuwasilisha kadi alama ya utekelezaji wa mkataba wa Lishe kwa kipindi cha miezi 6 (Julai- Desemba 2022), kutoa taarifa ya hali ya utekelezaji wa huduma za chanjo ikiwemo UVIKO-19 na kutoa elimu ya Bima ya Afya kwa wote.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yahaya Nawanda akizungumza wakati wa Kikao cha Tathmini ya Utekelezaji Mkataba wa Lishe, Chanjo na Bima ya Afya kwa Wote kilichohudhuriwa na wadau mbalimbali wa afya.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yahaya Nawanda akizungumza leo Alhamisi Februari 9,2023 wakati wa Kikao cha Tathmini ya Utekelezaji Mkataba wa Lishe, Chanjo na Bima ya Afya kwa Wote kilichohudhuriwa na wadau mbalimbali wa afya
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yahaya Nawanda akizungumza wakati wa Kikao cha Tathmini ya Utekelezaji Mkataba wa Lishe, Chanjo na Bima ya Afya kwa Wote kilichohudhuriwa na wadau mbalimbali wa afya.
Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Prof. Siza Tumbo akizungumza kwenye Kikao cha Tathmini ya Utekelezaji Mkataba wa Lishe, Chanjo na Bima ya Afya kwa Wote
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile akizungumza kwenye Kikao cha Tathmini ya Utekelezaji Mkataba wa Lishe, Chanjo na Bima ya Afya kwa Wote
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhee. Eliaas Ramadhani Masumbuko akizungumza kwenye Kikao cha Tathmini ya Utekelezaji Mkataba wa Lishe, Chanjo na Bima ya Afya kwa Wote
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akizungumza kwenye Kikao cha Tathmini ya Utekelezaji Mkataba wa Lishe, Chanjo na Bima ya Afya kwa Wote
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita akizungumza kwenye Kikao cha Tathmini ya Utekelezaji Mkataba wa Lishe, Chanjo na Bima ya Afya kwa Wote
Wadau wa afya wakiwa kwenye Kikao cha Tathmini ya Utekelezaji Mkataba wa Lishe, Chanjo na Bima ya Afya kwa Wote
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Mkude na Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita (kulia) wakisoma nyaraka kwenye Kikao cha Tathmini ya Utekelezaji Mkataba wa Lishe, Chanjo na Bima ya Afya kwa Wote
Wadau wa afya wakiwa kwenye Kikao cha Tathmini ya Utekelezaji Mkataba wa Lishe, Chanjo na Bima ya Afya kwa Wote
Wadau wa afya wakiwa kwenye Kikao cha Tathmini ya Utekelezaji Mkataba wa Lishe, Chanjo na Bima ya Afya kwa Wote
Wadau wa afya wakiwa kwenye Kikao cha Tathmini ya Utekelezaji Mkataba wa Lishe, Chanjo na Bima ya Afya kwa Wote
Mratibu wa Chanjo Mkoa wa Shinyanga, Timoth Sosoma akitoa taarifa ya hali ya utekelezaji wa huduma za chanjo ikiwemo UVIKO-19 kwenye Kikao cha Tathmini ya Utekelezaji Mkataba wa Lishe, Chanjo na Bima ya Afya kwa Wote
Afisa Lishe Mkoa wa Shinyanga, Yusuph Hamis akiwasilisha kadi alama ya utekelezaji wa mkataba wa Lishe kwa kipindi cha miezi 6 (Julai- Desemba 2022) kwenye Kikao cha Tathmini ya Utekelezaji Mkataba wa Lishe, Chanjo na Bima ya Afya kwa Wote
Meneja wa Bima ya Afya (NHIF) Mkoa wa Shinyanga Isack Katenda akitoa elimu ya Bima ya Afya kwa wote kwenye Kikao cha Tathmini ya Utekelezaji Mkataba wa Lishe, Chanjo na Bima ya Afya kwa Wote
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Girl Effect, Khalila Mbowe akielezea shughuli wanazofanya mkoani Shinyanga kwenye Kikao cha Tathmini ya Utekelezaji Mkataba wa Lishe, Chanjo na Bima ya Afya kwa Wote
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Girl Effect, Khalila Mbowe akielezea shughuli wanazofanya mkoani Shinyanga kwenye Kikao cha Tathmini ya Utekelezaji Mkataba wa Lishe, Chanjo na Bima ya Afya kwa Wote
Kaimu Meneja Mradi wa ACHIEVE Shinyanga unaotekelezwa na Shirika la NELICO kwa kushirikiana na Shirika la PACT, Fortunatus Richard akizungumza kwenye Kikao cha Tathmini ya Utekelezaji Mkataba wa Lishe, Chanjo na Bima ya Afya kwa Wote
Wadau wa afya wakiwa kwenye Kikao cha Tathmini ya Utekelezaji Mkataba wa Lishe, Chanjo na Bima ya Afya kwa Wote
Wadau wa afya wakiwa kwenye Kikao cha Tathmini ya Utekelezaji Mkataba wa Lishe, Chanjo na Bima ya Afya kwa Wote
Wadau wa afya wakiwa kwenye Kikao cha Tathmini ya Utekelezaji Mkataba wa Lishe, Chanjo na Bima ya Afya kwa Wote
Wadau wa afya wakiwa kwenye Kikao cha Tathmini ya Utekelezaji Mkataba wa Lishe, Chanjo na Bima ya Afya kwa Wote
Wadau wa afya wakiwa kwenye Kikao cha Tathmini ya Utekelezaji Mkataba wa Lishe, Chanjo na Bima ya Afya kwa Wote
Wadau wa afya wakiwa kwenye Kikao cha Tathmini ya Utekelezaji Mkataba wa Lishe, Chanjo na Bima ya Afya kwa Wote
Wadau wa afya wakiwa kwenye Kikao cha Tathmini ya Utekelezaji Mkataba wa Lishe, Chanjo na Bima ya Afya kwa Wote
Wadau kutoka Shirika la Girl Effect wakiwa kwenye Kikao cha Tathmini ya Utekelezaji Mkataba wa Lishe, Chanjo na Bima ya Afya kwa Wote
Wadau wa afya wakiwa kwenye Kikao cha Tathmini ya Utekelezaji Mkataba wa Lishe, Chanjo na Bima ya Afya kwa Wote
Wadau wa afya wakiwa kwenye Kikao cha Tathmini ya Utekelezaji Mkataba wa Lishe, Chanjo na Bima ya Afya kwa Wote
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yahaya Nawanda (kulia) akiwakabidhi cheti viongozi wa wilaya ya Kahama kutokana na kuibuka Washindi wa pili wa kwenye Mashindano ya usafi wa afya na mazingira kwa Hospitali za Wilaya nchini Tanzania. Aliyevaa kilemba ni Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yahaya Nawanda (kulia) akiwakabidhi cheti viongozi wa wilaya ya Shinyanga kutokana na kuibuka Washindi wa kwanza wa afya ya usafi na mazingira kwa Manispaa nchini Tanzania. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, Jomaary Satura akifuatiwa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Elias Ramadhan Masumbuko na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Johari Samizi.
Wadau wa afya wakiwa kwenye Kikao cha Tathmini ya Utekelezaji Mkataba wa Lishe, Chanjo na Bima ya Afya kwa Wote
Picha na Kadama Malunde – Malunde 1 blog