MKUU wa Wilaya ya Bahi Mhe.Godwin Gondwe,akizungumza wakati akifungua Kikao cha kamati ya lishe Mkoa cha robo Mwaka kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bi.Rosemary Senyamule kilichofanyika leo Februari 9,2023 jijini Dodoma.
KATIBU Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Dk Fatma Maganga,akizungumza wakati wa Kikao cha kamati ya lishe Mkoa cha robo Mwaka kilichofanyika leo Februari 9,2023 jijini Dodoma.
SEHEMU ya Viongozi Mkoa wa Dodoma wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Bahi Mhe.Godwin Gondwe,wakati akifungua Kikao cha kamati ya lishe Mkoa cha robo Mwaka kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bi.Rosemary Senyamule kilichofanyika leo Februari 9,2023 jijini Dodoma.
…………………….
Na Erick Mungele-DODOMA
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule,ameagiza elimu ya lishe iwe endelevu katika Wilaya zote kwa kushirikiana na Viongozi wote wa kata hadi ngazi za juu ili kufikia makundi mbalimbali katika mkoa wa Dodoma.
Maagizo hayo yametolewa leo Februari 9,2023 jijini Dodoma na Mkuu wa Wilaya ya Bahi Mhe.Godwin Gondwe kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wakati wa Kikao cha kamati ya lishe Mkoa cha robo Mwaka.
“Wajumbe hii elimu ya lishe iwe endelevu katika wilaya kwa kushirikiana na viongozi wote wa kata hadi nafasi za juu ili kufika makundi mabimbali katika mkoa wa Dododma,”amesama.
Aidha Gondwe amewataka maafisa elimu, kwenda kukagua mashamba ya shule yanaukubwa gani na kuagiza walime mazao ambayo watapata chakula kwa wingi shuleni lakini pia kwa kuwashirikisha maafisa ugavi ili wazazi wajifunze kupitia mshamba ya shule.
Kwa upande Mjumbe mmoja ,Maria Haule ameshauri viongozi wa Dini baada ya kupata elimu juu ya lishe watumie elimu hiyo kufikishia kwa waumini Makanisani na Misikitini maana wazazi wengi wamekuwa hawawapi watoto lishe bora na kufanya kazi za shamba zaidi.
“Ningependa kushauri viongozi wa dini watoe elimu juu ya lishe makanisani na misikitini maana kubaadhi ya wazazi wanajali shamba zaidi na wototo hawapati lishe bora,”amesema.