Katibu wa Askofu wa kanisa la Upendo wa Krsito Masihi lilillipo kijiji cha Milonde wilayani Tunduru Fulko Hyera akimuongoza Mhashamu Askofu wa kanisa hilo Noel Mbawala katika moja ya Ibaba maalum.
Mkuu wa wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma Wakili Julius Mtatiro kushoto akiwa na wawakilishi wa Askofu wa Kanisa la Upendo wa Kristo Masihi Kiuma,kulia katibu wa Askofu Fulko Hyera kulia.
Katibu wa Askofu wa Kanisa la Upendo Kristo Masihi Kiuma wilayani Tunduru Fulko Hyera wa pili kushoto na Katibu Mkuu wa taasisi ya Kiuma Daniel Malukuta katikati wakiwa katika picha ya na baadhi ya wafadhili wa kanisa hilo.
*******************
Na Muhidin Amri, Tunduru
KATIKA kuunga mkono jitihada za serikali za kuimarisha huduma za afya nchini,Kanisa la Upendo Kristo Masihi Kiuma,limetoa msaada wa vifaa tiba katika kituo cha Afya Mchoteka Halmashauri ya wilaya Tunduru mkoani Ruvuma ambacho ujenzi wake uko hatua ya mwisho kukamilika.
Akizungumza mbele ya Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Ruvuma Oddo Mwisho,Fulko Hyera kwa niaba ya Askofu Mkuu wa kanisa hilo Noel Mbawala, ametaja vifaa hivyo ni vitanda,shuka,magodoro na vifaa kwa ajili ya wananchi watakaofika kupata huduma za matibabu.
Aidha, amehaidi kupeleka wataalam wa ujenzi(mafundi)kuungana na waliopo ili ujenzi wa mradi huo ukamilike haraka na wananchi waanze kupate huduma na kuwaondolea adha ya kutembea umbali mrefu.
Hyera amesema,kanisa la Upendo wa Kristo Masihi linazalisha mafundi katika chuo chake cha ufundi kilicho chini ya taasisi ya Kiuma,hivyo wako tayari kutoa mafundi watakaokwenda kuisaidia serikali kuhusu mpango wake wa kujenga miradi yenye bora na viwango.
“Baba Askofu wa kanisa la Upendo wa Kristo Masihi anatambua Taifa letu linahitaji watu,akina mama watakaohitaji huduma ya kujifungua,wazee watatibiwa na hata vijana ambao ndiyo nguvu kazi nao watapata matibabu”alisema.
Amesema,wanatambua mchango na jitihada kubwa zinazofanywa na serikali ya awamu ya sita kwa kuwagusa na kuwajali wananchi kwa kutoa huduma muhimu za kijamii ikiwamo afya,elimu,maji na barabara ambazo zina mchango kubwa katika kukuza uchumi wa nchi yetu.
Amewapongeza viongozi wa serikali ya wilaya Tunduru wakiongozwa na mkuu wa wilaya hiyo Julius Mtatiro na mkoa wa Ruvuma kwa kusimamia na kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kwa manufaa ya wananchi.
Amesema,jitihada zinayofanywa na viongozi wa serikali iliyopo madarakani kutoa huduma bora za kijamii ni muhimu kuungwa mkono na wadau wengine wa maendeleo ikiwamo taasisi za Dini,badala ya kazi hiyo kufanywa na serikali pekee yake.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM mkoani Ruvuma Oddo Mwisho,amelipongeza kanisa hilo kwa kutambua jitihada zinazofanywa na serikali na kuwaomba wadau wengine kuungana na serikali yao ya Chama cha Mapinduzi za kuwaleta maendeleo wananchi.