Kufuatia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kumteua Prof. Verdiana Grace Masanja kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI), Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi H. Chana (Mb) kwa mamlaka aliyopewa chini ya Kifungu cha 6(1) cha Sheria ya Utafiti wa Misitu Tanzania Na.5 ya Mwaka 1980, amewateua wafuatao kuwa wajumbe wa Bodi ya Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI) :-
- Prof. Dos Santos Silayo, Kamishna wa Uhifadhi, Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS).
- Bw. Daniel Charles Pancras, Kaimu Mkurugenzi Msaidizi, Maendeleo ya Ufugaji Nyuki, Wizara ya Maliasili na Utalii.
- Prof. Faustin Rweshabura Kamuzora, Profesa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA).
- Dkt. Zanifa Omary, Mhadhiri, Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM).
- CPA. Beatrice Musa Lupi, Mkurugenzi wa Fedha, Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF).
- Dkt. Hulda Gideon Mapunjo, Afisa Uratibu wa Utafiti Mkuu, Tume ya Sayansi na Teknolojia Tanzania (COSTECH).
- Bw. John John Nchimbi, Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto.
- Adv. Xavier Masalu Ndalahwa, Wakili wa Serikali wa Mkoa wa Morogoro, Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali.
Aidha, Dkt. Revocatus Petro Mushumbusi, Mkurugenzi Mkuu, Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI) anakuwa katibu wa Bodi hiyo. Uteuzi huu ni wa miaka mitatu kuanzia tarehe 30 Januari, 2023 hadi 31 Januari, 2026.