Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM na mlezi wa Mkoa wa Dodoma Bi, Leila Ngozi,akizungumza wakati wa maadhimisho ya miaka 46 ya Chama cha Mapinduzi katika kata ya Ipera Halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa Jijini Dodoma.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM na mlezi wa Mkoa wa Dodoma Bi, Leila Ngozi,akisisitiza jambo wakati wa maadhimisho ya miaka 46 ya Chama cha Mapinduzi katika kata ya Ipera Halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa Jijini Dodoma.
Sehemu ya Viongozi wa Chama wakimsikiliza Mlezi wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dodoma na Mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa Bi, Leila Ngozi,(hayupo pichani) wakati wa maadhimisho ya miaka 46 ya Chama cha Mapinduzi katika kata ya Ipera Halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa Jijini Dodoma.
Mbunge wa Jimbo la Kibakwe ambaye pia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene,akizungumza wakati wa maadhimisho ya miaka 46 ya Chama cha Mapinduzi katika kata ya Ipera Halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa Jijini Dodoma.
Mbunge wa Jimbo la Kondoa Vijijini ambaye pia ni Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji ,akizungumza wakati wa maadhimisho ya miaka 46 ya Chama cha Mapinduzi katika kata ya Ipera Halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa Jijini Dodoma.
Mbunge wa Jimbo la Kongwa ambaye pia ni Spika Mstaafu Mhe.Job Ndugai,akizungumza wakati wa maadhimisho ya miaka 46 ya Chama cha Mapinduzi katika kata ya Ipera Halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa Jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dodoma Alhaji Adam Kimbisa ,akizungumza wakati wa maadhimisho ya miaka 46 ya Chama cha Mapinduzi katika kata ya Ipera Halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa Jijini Dodoma.
KATIBU wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Mkoa wa Dodoma Pili Mbanga,akizungumza wakati wa maadhimisho ya miaka 46 ya Chama cha Mapinduzi katika kata ya Ipera Halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa Jijini Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Sitaki Senyamule, ,akizungumza wakati wa maadhimisho ya miaka 46 ya Chama cha Mapinduzi katika kata ya Ipera Halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa Jijini Dodoma.
…………………………………..
Na Mwandishi wetu-MPWAPWA
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM na mlezi wa Mkoa wa Dodoma Bi, Leila Ngozi ametoa rai kwa viongozi wa serikalikuendelea kutenga muda kwa ajili kusikiliza na kutatua changamoto za wananchi.
Wito huo umetolewa wakati wa kumbukumbu ya miaka 46 ya Chama cha mapinduzi iliyofanyika katika kata ya Ipera Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Jijini Dodoma.
Mlezi wa Chama cha Mapinduzi Bi, Leila ameomba viongozi kuendelea kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi ambayo wanaccm wanajivunia imefanya mambo mengi.
Ameongeza kusema Ilani imeelekeza katika sura ya 10 ibara ya 251, “kuwa tunatakiwa tutenge muda wakwenda kusikiliza wananchi wetu, Niwaombe wananchi tuendelee kueleza changamoto zetu kwa viongozi wetu ili waweze kuzifanyia kazi,” alisema Bi, Leila.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dodoma Alhaji Adam Kimbisa ametoa rai kwa watendaji wa Serikali kutenda haki katika maamuzi na kuepuka dhuluma na uonevu.
“Wanachi toeni taarifa kama kuna mienendo isiyofaa kwa watendaji wa serikali katika kutoa huduma,” alisema Alhaj Kimbisa
Awali Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe, Rosemary Senyamule amesema ilani ya Chama cha Mapinduzi inatekelezeka kwa kasi kubwa kutokana na dhamira ya dhati ya Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Taifa ambaye pia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
“Upo mradi mkubwa wa umwagiliaji ambao upo katika hatua nzuri ya ujenzi, na mradi wa ukarabati wa Hospitali ya wilaya ya Mpwapwa ambao umeshakamilika na Mheshimiwa Rais ameridhia ujenzi wa barabara ya lami ili kuunganisha barabara wilaya ya Mpwapwa kwa lami,” alisema Mkuu wa Mkoa.
Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu (Mb) wa Kibakwe Mhe. George Simbachawene amesema furaha ya watu wa Ipera ni kukamilika wa kituo cha afya cha Ipera.
“Tunajivunia maendeleo lakini lazima tuendele kufanya kazi na tujitegemee katika kujenga taifa,” alisema waziri Simbachawene.