MKURUGENZI Mtendaji wa Hospital ya Benjamin Mkapa .Dkt.Alphonce Chandika wakisaini makubaliano ya ushirikiano wa kutoa huduma za upasuaji wa moyo kwa watoto na shirika lisilo la kiserikali la Childrens Heart Charity Association la nchini Kuwaita.
MKURUGENZI Mtendaji wa Hospital ya Benjamin Mkapa .Dkt.Alphonce Chandika wakibadilishana nyaraka na Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kutoka shirika la children heart charity association la nchini Kuwaiti Dkt.Faisal Al-Saeed mara baada ya kusaini makubaliano ya ushirikiano wa kutoa huduma za upasuaji wa moyo kwa watoto na shirika lisilo la kiserikali la Childrens Heart Charity Association la nchini Kuwait.
MKURUGENZI Mtendaji wa Hospital ya Benjamin Mkapa .Dkt.Alphonce Chandika ,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kusaini makubaliano ya ushirikiano wa kutoa huduma za upasuaji wa moyo kwa watoto na shirika lisilo la kiserikali la Childrens Heart Charity Association la nchini Kuwait.
MKURUGENZI Msaidizi kutoka wizara ya afya Dk. Caroline Damian,akizungumza mara baada ya kushuhudia makubaliano ya ushirikiano wa kutoa huduma za upasuaji wa moyo kwa watoto na shirika lisilo la kiserikali la Childrens Heart Charity Association la nchini Kuwait.
BALOZI wa Tanzania nchini Kuwait Mhe.Said Mussa,akizungumza mara baada ya kushuhudia makubaliano ya ushirikiano wa kutoa huduma za upasuaji wa moyo kwa watoto na shirika lisilo la kiserikali la Childrens Heart Charity Association la nchini Kuwait.
…………………………..
Na.Alex Sonna-DODOMA
HOSPITALI ya Kanda ya Benjamin Mkapa (BMH) imeingia makubaliano ya ushirikiano wa kutoa huduma za uchunguzi na upasuaji wa moyo kwa watoto na Shirika lisilo la kiserikali la Children’s Heart Association la Nchini Kuwait.
Hafla ya utiaji saini makubaliano hayo imefanyika leo Februari 6,2023 jijini Dodoma na kushuhudiwa na Balozi wa Tanzania nchini Kuwait Mheshimiwa Said Shaibu Mussa.
Akizungumza mara baada ya makubaliano hayo Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa Dkt. Alphonce Chandika amesema kuwa katika makubaliano hayo Shirika la Children’s heart litagharamia matibabu ya moyo kwa watoto wenye matatizo yanayohitaji upasuaji pamoja na kusaidia vifaa vinavyohiotajika kuwezesha matibabu hayo ili kuyafanya yawe endelevu.
Aidha Dkt Chandika amesema kuwa pamoja na huduma hizo za upasuaji madaktari hawa kutoka nchini Kuwait watasaidia kuwajengea uwezo madaktari, wauguzi na wataalamu wa huduma za uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya moyo ili kuwawezesha kuendelea kutoa huduma hizo kwa ufanisi na kwa kutumia teknolojia mpya.
“Madaktari wetu wazawa kutoka BMH wanaenda kupata ujuzi, kama ilivyookuwa kwa madktari wa Figo, wajerumani walikuja wakawajengea uwezo na sasa wanapandikiza figo wenyewe, hata hawa wa moyo watajengewa uwezo na hatimae watakuwa wanafanya upasuaji wa moyo wao wenyewe” amesema Dkt. Chandika.
Dkt Chandika amesema kuwa madaktari kutoka nchini Kuwait tayari wamefika BMH kuanzia tarehe 3 mwezi huu na tayari wamefanya upasuaji kwa watoto wawili na huduma itaendelea hadi Februari 9 ambapo wanategemea kuhudumia watoto Zaidi ya 100.
“Tunashukuru Shirika hili kwa mwitikio wao, tumeanza mazungumzo nao mwaka jana mwezi novemba lakini mwaka huu mwezi wa pili tayari wamefika na kuanza kuwahudumia watoto”
Amesema kuwa Dodoma kijiografia iko katikati ya Tanzania, kwa hiyo kujenga kituo cha matibabu hapa kutasaidia wagonjwa kufika kupata huduma kwa urahisi, kutoka Mwanza ambako ndio magonjwa haya ya moyo yameshamiri kuja Dodoma ni karibu kuliko kwenda Dar es salaam, kutoka Mbeya, Kigoma ni rahisi pia kuja Dodoma.
“Katika kuendana na azma ya Muheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kutamani kuona watanzania tunaenda kwenye utalii wa matibabu, sisi BMH tumelitekeleza hilo, tunawaita madaktari kutoka nje na tunaboresha huduma pia” amesema
Kwa upande wake Balozi wa Tanzania nchini Kuwait Mhe. Said Mussa mesema kuwa makubaliano ya ushirikiano na Children’s Heart Charity yalianza mwaka jana mwezi Novemba katika Hospitali ya Muhimbili na sasa mkazo zaidi umewekwa BMH ili kuwasaidia watoto wengi kutoka mikoani hasa katika mikoa ya kanda ya ziwa waweze kufika kupata huduma kwa urahisi.
“Sisi tunaofanya kazi nje kwa niaba ya nchi tuna wajibu wa kutafuita fursa za kiuchumi, kibiashara na uwekezaji lakini katika utekelezaji wa diplomasia ya Uchumi suala la huduma ya jamii lina mchango mkubwa” amesema Mhe.Mussa
Naye Daktari Bingwa wa Magonjwa ya moyo kutoka shirika la children heart charity association la nchini Kuwaiti Dkt.Faisal Al-Saeed,amesema kuwa wanaimani malengo wanayotarajia kuyafikia yatafanikiwa kwa sababu wamepata ushirikiano mkubwa kutoka kwa uongozi wa Benjamin Mkapa.
Makubaliano haya yatadumu kwa muda wa miaka mitatu na kutoa fursa Zaidi kwa madaktari wetu wazawa kujifunza Zaidi.