Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM),Itikadi na Uenezi Sophia Mjema,Akizungumza na wananchi wa Mikese baada ya kufanya ziara katika Kituo cha Afya Mikise mkoani Morogoro.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndg. Daniel Chongolo akipatiwa maelezo ya Vifaa Kwenye Chumba cha Upasuaji na Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro Dkt. Robart Manyerere alipofanya ziara ziara katika Kituo cha Afya Mikise mkoani Morogoro.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndg. Daniel Chongolo Akizungumza na wananchi wa Mikese baada ya kufanya ziara katika Kituo cha Afya Mikise mkoani Morogoro katika Ziara ya Kukagua, Kuhimiza na Kusimamia Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Akizungumza na Mwenyekiti wa Shina Namba 1, kata ya Ngerengere Ndugu Salum Rashid, katika Ziara ya Kukagua, Kuhimiza na Kusimamia Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025,Wilaya ya Morogoro mkoani Morogoro.
Wananchi wa Mikese wakinyanyua Mkono kuzungumzia Changamoto Zao Kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Daniel Chongolo wakati Akizungumza na wananchi wa Mikese baada ya kufanya ziara katika Kituo cha Afya Mikise mkoani Morogoro. (Picha Zote na Fahadi Siraji CCM)
…………………………………….
CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) kimesisitiza moja ya mikakati ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dk.Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha huduma za afya hasa ya Mama na Mtoto inaendelea kuboreshwa ili wapate huduma zilizo bora zinazoambatana na vifaa tiba vya kisasa.
Akizungumza leo Februari 4,2023 na wananchi wa Mikese baada ya kufanya ziara katika Kituo cha Afya Mikise mkoani Morogoro , Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM),Itikadi na Uenezi Sophia Mjema amesema lengo mojawapo la Serikali ya Chama hicho ni kuboresha huduma za afya kwa kutoa huduma bora na vifaa tiba vilivyobora.
“Katika Kituo cha Afya Mikese tumeona jengo la Mama na Mtoto lakini tumeona vifaa tiba ambavyo ni bora na vya kisasa kabisa kikiwemo kitanda cha kujifungulia , akina mama mnajua ukishapata uchungu unakaa unahangaika hangaika lakini kitanda chenyewe kinakwambia geuka kulia, geuka kushoto , kwa hiyo wanawake wanajifungua kwa raha.
“Yote hayo yanafanyika kwa sababu ya Rais Samia Suluhu Hassan lakini kwa namna ambavyo Serikali imeamua kuboresha huduma za mama na mtoto baada ya mama kujifungua anakwenda kwenye eneo maalum kwa ajili ya kuangalia afya zao kama ziko vizuri lakini hata akienda nyumbani bado kuna utaratibu wa kufuatilia ili kujua maendeleo. Yote hayo yanafanyika chini ya Chama Cha Mapinduzi(CCM),”amesema Mjema.
Ameongeza Serikali ya Awamu ya Sita inataka kuona mama anajifungua vizuri na aendelee kukuwa akiwa na akili zake vizuri huku akitumia nafasi hiyo kukumbusha wazazi kuzingatia siku 1000 katika kumlea mtoto ikiwa pamoja na kunyonyweshwa vizuri na kulishwa vizuri na kupata virutubisho.
“Mtoto akitoka hapo hao ndio wanakuwa ma-genius(vipaji) wa baadae kwa hiyo akina baba , akina mama tuhakikishe tunasomesha watoto wetu lakini tunahakikisha tunamsomea mtoto wa kike vizuri zaidi ,mtoto wa kike ana kumbuka nyumbani , kwa hiyo haya yote yanayofanyika katika huduma za afya ni kwa ajili ya kuhakikisha tunamsaidia mama anayeleta binadamu mwingine kwenye dunia hii
“Lakini katika kuhakikisha binadamu huyo anakuwa vizuri ni jambo la kuweka mikakati kwamba binadamu huyu anayezaliwa Tanzania azaliwe vizuri, alelewe vizuri kwenye zile sikue 1000 zake na apate lishe nzuri baada ya hapo atakapokuwa ndipo tutakuwa na watu wenye akili watakaotoka hapa Tanzania.
“Ili tufike huko lazima kuwepo na mikakati ikiwemo ya kuboresha huduma za afya ya mama na mtoto.Mama Samia ni mama mikakati na anaona mbali na anajua akikutayarisha hivi baadae nchi itakuwa inaongoza Afrika lakini duniani , tunataka tukimbie twende katika nchi ambazo zimeendelea zaidi,”amesema Mjema.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi ameongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndugu Sophia Mjema, Katibu wa NEC Oganaizesheni Ndugu Issa Ussi (Gavu) pamoja na Viongozi na Watendaji wa Chama na Serikali ambapo ziara hii ina lengo la Kukagua, Kuhimiza na Kusimamia Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025