Muonekano wa Kanisa la EAGT Mshikamano kata ya Ngokolo Manispaa ya Shinyanga lililoanguka kufuatia mvua ya upepo iliyonyesha Februari 2,2023
Kaimu Meneja TANESCO Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Leo Mwakatobe akionesha miundombinu ya umeme iliyoharibika kufuatia mvua ya upepo kuangusha mti katika eneo la Mshikamano kata ya Ngokolo Manispaa ya Shinyanga
Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Mvua kubwa iliyoambatana na Upepo imeharibu Miundo mbinu ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) mkoa wa Shinyanga na kusababisha kukosekana kwa huduma ya umeme na mapato huku ikiharibu majengo ya wananchi wakiwemo wateja wa TANESCO.
Akizungumza leo Ijumaa Februari 3,2023 wakati akitembelea maeneo yaliyoathirika na mvua hiyo ya upepo, akiwa ameambatana na Mhandisi Mkuu wa TANESCO Shinyanga, Kurwa Mangara na Afisa Mahusiano na Huduma kwa wateja Lilian Mungai, Kaimu Meneja TANESCO Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Leo Mwakatobe amesema miundombinu ya umeme iliyoharibika ni ya Mjini Shinyanga na Njia kuu ya umeme kutoka kituo cha kupooza umeme cha Ibadakuli kwenda Usanda, Tinde hadi Luhumbo.
“Mvua iliyoambatana na upepo iliyonyesha jana Alhamisi Februari 2,2023 majira ya saa 11 jioni imeharibu miundombinu ya umeme sehemu nyingi za Mjini Shinyanga na kusababisha TANESCO kukosa mapato yatokanayo na huduma ya kusambaza umeme lakini pia wateja wetu kukosa huduma ya umeme kwa sababu upepo huo uliangusha nguzo za umeme, ulivunja miti na miti hiyo kuangukia nyaya za umeme na kuvunja vyuma vya kupokelea umeme kutoka kwenye nguzo hadi kwenye nyumba”,amesema Mhandisi Mwakatobe.
“ Tunamshukuru Mwenyezi Mungu mvua hiyo iliyoambatana na upepo haikuleta madhara kwa binadamu kwani kitengo chetu cha Dharura kilichukua hatua ya haraka kufuatia mvua hiyo ya umeme. Mvua hiyo imesababisha uharibifu wa nyumba za wateja wetu ikiwemo kuanguka na mapaa kuezuliwa na kukosa huduma ya umeme”,ameeleza Mhandisi Mwakatobe.
Hata hivyo amesema tayari wamesharudisha huduma ya umeme kwenye maeneo mengi na wanaendelea kurejesha huduma ya umeme kwenye maeneo yaliyoathirika zaidi Mjini Shinyanga.
Kwa upande wake Mhandisi Mkuu wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga Kurwa Mangara amesema mvua hiyo iliyoambatana na upepo ilisababisha miti kuanguka huku akiyataja maeneo yaliyoathirika zaidi kuwa ni Chamaguha, Ngokolo na Lubaga pamoja na maeneo yaliyopo kwenye Njia Kuu ya Umeme kutoka Ibadakuli kwenda Luhumbo ambayo ni Kitangili, Usanda, Nhelegani, Ishinabulandi, Tinde, Luhumbo, Welezo, Puni, Nyashimbi, Zobogo na Ihalo.
Nao baadhi ya wananchi walioathiriwa na mvua hiyo akiwemo Said Hussein na Mchungaji wa Kanisa la EAGT Mshikamano kata ya Ngokolo Manispaa ya Shinyanga, Daniel Emmanuel Manga wamesema majengo yao yameharibika kutokana na mvua hiyo huku wakiishukuru TANESCO kuzima umeme haraka hali iliyosababisha kusiwe na madhara ya kibinadamu.
“Mvua hiyo ya upepo imeangusha Kanisa letu la EAGT ambalo tulilokuwa tunaendelea kujenga likiwa tayari limeshawekewa paa. Kanisa hili lina uwezo wa kuchukua waumini 1000 kwa wakati mmoja na mpaka sasa gharama tulizotumia ni takribani Shilingi Milioni 100, kwa kweli tumepata hasara kubwa,paa limeanguka na sehemu ya kanisa imebomoka. Tunashukuru hapakuwa na watu ndani ya kanisa muda huo”, amesema Mchungaji Manga.
Kaimu Meneja TANESCO Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Leo Mwakatobe akionesha nguzo za umeme zilizoanguka katika eneo la Nhelegani Manispaa ya Shinyanga kufuatia mvua iliyoambatana na upepo Februari 2,2023. Picha na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Kaimu Meneja TANESCO Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Leo Mwakatobe akionesha nguzo za umeme zilizoanguka katika eneo la Nhelegani Manispaa ya Shinyanga kufuatia mvua iliyoambatana na upepo Februari 2,2023.
Zoezi la kuchimba mashimo kwa ajili ya kuweka nguzo mpya za umeme likiendelea katika eneo la Nhelegani Manispaa ya Shinyanga.
Muonekano wa Nguzo za umeme zilizoathiriwa na Mvua ya upepo katika eneo la Iwelyangula kata ya Chamaguha Manispaa ya Shinyanga
Muonekano wa Nguzo za umeme zilizoathiriwa na Mvua ya upepo katika eneo la Iwelyangula kata ya Chamaguha Manispaa ya Shinyanga
Fundi wa TANESCO akiendelea na kazi ya kutengeneza miundombinu ya umeme katika eneo la Iwelyangula kata ya Chamaguha Manispaa ya Shinyanga
Fundi wa TANESCO akiendelea na kazi ya kutengeneza miundombinu ya umeme katika eneo la Iwelyangula kata ya Chamaguha Manispaa ya Shinyanga
Mafundi wa TANESCO wakiendelea na kazi ya kutengeneza miundombinu ya umeme katika eneo la Iwelyangula kata ya Chamaguha Manispaa ya Shinyanga
Mafundi wa TANESCO wakiendelea na kazi ya kutengeneza miundombinu ya umeme katika eneo la Iwelyangula kata ya Chamaguha Manispaa ya Shinyanga
Kaimu Meneja TANESCO Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Leo Mwakatobe (katikati), Mhandisi Mkuu wa TANESCO Shinyanga, Kurwa Mangara (kulia) na Afisa Mahusiano na Huduma kwa wateja Lilian Mungai wakiangalia nguzo ya umeme iliyoathiriwa na mvua ya upepo kwenye nyumba ya mteja wa TANESCO eneo la Buhangija Mjini Shinyanga
Kaimu Meneja TANESCO Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Leo Mwakatobe akionesha miundombinu ya umeme iliyoharibika kufuatia mvua ya upepo kuangusha mti katika eneo la Mshikamano kata ya Ngokolo Manispaa ya Shinyanga
Kaimu Meneja TANESCO Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Leo Mwakatobe akionesha miundombinu ya umeme iliyoharibika kufuatia mvua ya upepo kuangusha mti katika eneo la Mshikamano kata ya Ngokolo Manispaa ya Shinyanga
Muonekano wa Kanisa la EAGT Mshikamano kata ya Ngokolo Manispaa ya Shinyanga lililoanguka kufuatia mvua ya upepo iliyonyesha Februari 2,2023
Muonekano wa Kanisa la EAGT Mshikamano kata ya Ngokolo Manispaa ya Shinyanga lililoanguka kufuatia mvua ya upepo iliyonyesha Februari 2,2023
Muonekano wa Kanisa la EAGT Mshikamano kata ya Ngokolo Manispaa ya Shinyanga lililoanguka kufuatia mvua ya upepo iliyonyesha Februari 2,2023
Mchungaji wa Kanisa la EAGT Mshikamano kata ya Ngokolo Manispaa ya Shinyanga, Daniel Emmanuel Manga akielezea jinsi mvua ya upepo ilivyoharibu kanisa hilo.
Muonekano wa Kanisa la EAGT Mshikamano kata ya Ngokolo Manispaa ya Shinyanga lililoanguka kufuatia mvua ya upepo iliyonyesha Februari 2,2023
Muonekano wa Kanisa la EAGT Mshikamano kata ya Ngokolo Manispaa ya Shinyanga lililoanguka kufuatia mvua ya upepo iliyonyesha Februari 2,2023
Muonekano wa Kanisa la EAGT Mshikamano kata ya Ngokolo Manispaa ya Shinyanga lililoanguka kufuatia mvua ya upepo iliyonyesha Februari 2,2023
Mhandisi Mkuu wa TANESCO Shinyanga, Kurwa Mangara akionesha mita na chuma cha kupokelea umeme kutoka kwenye nguzo kwenda kwenye nyumba ya mkazi wa Lubaga Mjini Shinyanga baada ya kuathiriwa na mvua ya upepo. Kushoto ni Afisa Mahusiano na Huduma kwa wateja Lilian Mungai katikati ni Kaimu Meneja TANESCO Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Leo Mwakatobe
Zeozi la kurejesha huduma ya umeme likiendelea katika eneo la Lubaga Mjini Shinyanga
Zeozi la kurejesha huduma ya umeme likiendelea katika eneo la Lubaga Mjini Shinyanga .
Picha na Kadama Malunde – Malunde 1 blog