Katibu Mkuu ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tamisemi Profesa Riziki Shemdoe ameziagiza Halmashauri zote nchini zianze kufanya miradi ya uwekezaji ili kuziwezesha Halmashauri hizo kuongeza mapato na kuondokana na utegemezi mkubwa wa bajeti ya serikali kuu ili kuendesha shuguli zake.
Profesa Shemdoe alitoa agizo hilo mkoani Morogoro wakati akifungua mafunzo ya siku kumi kwa maafisa mipango kutoka katika Halmashauri kumi na tatu (13) ili kuwajengea uwezo wa kuandika miradi mikubwa na inayokopesheka na ambayo pia itaweza kusaidia kuongeza uwezo wa Halmashauri husika kukusanya mapato ya kutosha kwa ajili ya maendeleo.
Aidha Profesa Shemdoe amesema uanzishwaji wa miradi hiyo mikubwa inalenga kuongeza wigo wa ajira kwa watanzania na hivyo kupunguza malalamiko dhidi ya Serikali juu ya ukosefu wa ajira kwa vijana licha ya kuwa Halmashauri zitakuwa zimeongeza pia ukusanyaji wa mapato pamoja sambamba na kutoa gawio kwa serikali kuu.
“Kwa sasa Halmashauri zinazokusanya zaidi ya bilioni 10 ni chache sana ukilinganisha na idadi ya halmashauri tulizonanzo nchini laakini kikubwa ni kwamba kama tutatengeneza miradi ambayo tunaweza hata kuipangisha kasha fedha zote zikalipwa kwenye halamashari itakuwa na manufaa makubwa sana”alisema Profesa Shemdoe.
Kwa upande wake Makamo Mkurugenzi Chuo cha Mipango Kanda ya Ziwa Profesa Jvenal Nkwazoki alisema kuwa ipo haja ya kupeleka mafunzo hao kwa watoa maamuzi ili kuweka uelewa wa pamoja katika kupanga na kuamua miradi yenye manufaa kwa halmashauri husika.
Naye muwezeshaji wa mafunzo hayo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea Dokta Frederick Sagamiko alisema kuwa faida zaidi zitakazo patikana kwenye mfumo ni halmashau kuanzisha miradi ya uwekezaji ni kwamba miradi hiyo itasimamiwa na wataalamu na kuongeza ajira kwa maafisa masoko ambao hata hivyo kwa sasa hakuna halmashauri iliyoajiri afisa masoko.
Dokta Bonimass Mbasa mhadhiri mwandamizi chuo cha mipango ya maendeleo vijijini alisema kuwa mafunzo hayo yatapelekwa kwenye halmashauri zonte nchini na kwa maafisa mipango nchi nzima pamoja na wakurugenzi wote wa ahalamashauri ili kuwajengea uwezo wa namna bora ya uanzishaji wa kampuni ili waweze kukopa na kupata fedha za uendeshaji wa kampuni hizo.