*****************
Na Lucas Raphael,Tabora
Watumishi watatu wa halmashauri ya wilaya nzega mkoani Tabora wamefikishwa mahakamani na Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU kwa tuhuma za uhujumu uchumi .
Akisoma mashitaka hayo leo mbele ya hakimu mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Nzega Hudi Majid Hudi mwendesha mashitaka wa Takukuru Mizengo Joseph aliambia mahakama hiyo kwamba Watumishi hao wakiwa waajiriwa wa serikali wanakabiliwa na mshitaka matatu .
Aliimbia mahakama hiyo kwamba watumishi hao wanakabiliwa na shitaka la kutumia nyaraka kumdanganya mwaajiri,kula njama na kutenda kosa,na ubadhirifu
Mwendesha mashitaka huyo aliwataja watumishi hao kuwa ni Dkt aliyekuwa zamu siku ya tukio John nyeho (34)Justina Kashinhi(38)na afisa manunuzi Andrew Shillah ambaye ni Fundi.
Mizengo aliendelea kuiambia mahakama hiyo kwamba kati ya juni 10 hadi 25 mwaka 2020 kwa muda tofauti tofauti wakiwa katika ofisi ya Halmashauri ya nzega walitumia nyaraka zenye maelezo ya uongo kuwa wametumia kiasi cha shilingi milioni 6,360,000/ kwa ajili ya malipo ya X-Rey Mashine.
Alisema kwamba huku wakijua kabisa X-Rey Mashine haikutengenezwa kwa gharama hiyo hivyo kufanya ubadhirifu wa kiasi hicho cha fedha za serikali .
Mizengo alisema kwamba washitakiwa wote watatu walitendo makosa hayo kinyume na kifungu cha 22 cha sheria ya kuzuia na kupambana na Rushwa marejeo ya mwaka 2022.
Washitakiwa baada ya kusomewa mashitaka wote walikana kuhusika na tuhuma hizo na wapo nje kwa dhamana ya shilingi milioni tatu kwa maneno kwa kila moja na wadhimini wawili na kesi imehairishwa hadi februal 16 mwaka huu.