Mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela akizungumza katika halfa ya kuwaapisha wakuu wapya wa wilaya za mkoa wa Arusha.
Wakuu wapya wa wilaya tatu za mkoa wa Arusha wakimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Arusha wakati wakiapishwa leo jijini Arusha.
Mkuu mpya wa wilaya ya Arumeru, Emmanuela Kaganda akila kiapo wakati akiapishwa mkoani Arusha leo.
Mkuu mpya wa wilaya ya Arusha akila kiapo wakati wa kuapishwa leo jijini Arusha.
**************************
Julieth Laizer ,Arusha.
MKUU wa mkoa wa Arusha, John Mongela,amewataka wakuu wapya wa wilaya Mkoani humo, kuacha mihemko ya kukimbilia kuwakamata wananchi na kuwaweka ndani badala yake wajifunze kuongoza bila kutumia vyombo vya dola.
Aidha amewapongeza waliokuwa wakuu wa Wilaya za ,Arumeru, Mhandisi Richard Ruyango na mkuu wa Wilaya ya Monduli, Frank Mwaisumbe ambao wamestaafu utumushi wao bila kuwa na uongozi wenye mihemko.
Kauli hiyo ameisema leo jijini Arusha wakati akiwaapisha wakuu wapya, Felician Gaspar Mtahengerwa(Arusha),Emmanuela Kaganda(Arumeru), Suleiman Mwenda (Monduli)ambaye alikuwa mkuu wa wilaya ya Iramba mkoani Singida,na Marko Ng’umbi , (Longido), ambao waliteuliwa wiki iliyopita.
Amesema kuwa wakuu hao wa Wilaya wanapaswa kufuata kanuni na sheria za utawala wa kisheria na kujitenga na utawala wa kutumia mabavu na vyombo vya dola. “Mnaniona mimi sina tabia ya kuweka ndani wa