Mwenyekiti wa kijiji cha Uwimba Bwana Richard Kalekene akitoa maelezo ya namna Wananchi wa kijiji hicho waliupokea Mradi wa REA III, Mzunguko wa Pili akiwa ofisini kwake anaotazama nao ni Mjumbe wa Bodi ya Nishati (Katikati) Bwana Florian Haule na Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi kutoka REA, Mhandisi Jones Olotu (Mwenye flana ya bluu) wengine ni Augustino Lyimo Msimamizi wa Mradi, Mhandisi wa Miradi ya REA mkoa wa Mbeya, Mhandisi Hamis Mrope, Mhandisi wa Miradi ya REA mkoa wa Rukwa na Katavi, Mhandisi Dunstan Kalugira na wengine ni Mhandisi Mustapha Himba na Mwakilishi wa Menejimenti Bwana Dude Fuime wote kutoka ETDCO
Mhandisi Jones Olotu (Mwenye flana ya bluu) akitoa maelezo pembeni yake ni Mjumbe wa Bodi ya Nishati (Katikati) Bwana Florian Haule wengine ni Augustino Lyimo Msimamizi wa Mradi, Mhandisi wa Miradi ya REA mkoa wa Mbeya, Mhandisi Hamis Mrope, Mhandisi wa Miradi ya REA mkoa wa Rukwa na Katavi, Mhandisi Dunstan Kalugira na wengine ni Mhandisi Mustapha Himba na Mwakilishi wa Menejimenti Bwana Dude Fuime wote kutoka ETDCO.
Ujumbe kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA) pamoja na timu ya Mkandarasi (Kampuni ya ETDCO) wakimsikiliza Mwenyekiti wa kijiji cha Uwimba Bwana Richard Kalekene akitoa maelezo ya namna Wananchi wa kijiji hicho waliupokea Mradi wa REA III, Mzunguko wa Pili akiwa ofisini kwake, hivi karibuni.
Ujumbe wa REA ukiongozwa na Mjumbe wa Bodi ya Nishati, Bwana Florian Haule wakimsikiliza Mhandisi Mustapha Himba, Meneja wa Mradi REA III, Mzunguko wa Pili kutoka ETDCO wakiwa eneo la Mradi katika kijiji cha Uwimba, wilaya ya Mbeya vijijini, hivi karibuni.
Ujumbe wa REA ukiongozwa na Mjumbe wa Bodi ya Nishati, Bwana Florian Haule wakimsikiliza Mhandisi Mustapha Himba, Meneja wa Mradi REA III, Mzunguko wa Pili kutoka ETDCO wakiwa eneo la Mradi katika kijiji cha Uwimba, wilaya ya Mbeya vijijini, hivi karibuni.
Ujumbe wa REA ukiongozwa na Mjumbe wa Bodi ya Nishati, Bwana Florian Haule wakiangalia ubora wa nguzo zilizotumika kupitisha nyaya kwenye Mradi REA III, Mzunguko wa Pili kutoka ETDCO wakiwa eneo la kijiji cha Uwimba, wilaya ya Mbeya vijijini, hivi karibuni.
Kutoka kushoto Mhandisi wa Miradi ya REA mkoa wa Mbeya, Mhandisi Hamis Mrope, Mhandisi wa Miradi ya REA mkoa wa Rukwa na Katavi, Mhandisi Dunstan Kalugira na wengine ni Mwakilishi wa Menejimenti Bwana Dude Fuime kutoka ETDCO akiwa pamoja na Mjumbe wa Bodi ya Nishati Bwana Florian Haule n Bwana Augustino Lyimo Msimamizi wa Mradi (ETDCO) akiwa pamoja na Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi, Mhandisi Jones Olotu wakimsikiliza Mhandisi Mustapha Himba, Meneja wa Mradi kutoka ETDCO
X8. Sehemu ya miundombinu ya umeme wa Mradi wa REA III, Mzunguko wa Pili katika kijiji cha Uwimba, kata ya Swaya, wilaya ya Mbeya vijijini
……………….
Ujumbe wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) ukiongozwa na Mjumbe wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB) Bwana Florian Haule hivi karibuni umetembelea kijiji cha Wimba kilichopo kwenye Kata ya Swaya wilaya ya Mbeya vijijini ili kutathmini maendeleo ya Mradi wa kusambaza umeme wa REA III, Mzunguko wa Pili ambapo zaidi ya Wateja wa awali 42 wataunganishwa na huduma ya umeme, mwezi Februari, 2023.
Katika msafara huo alikuwepo pia Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi kutoka REA, Mhandisi Jones Olotu, Mhandisi wa Miradi ya REA mkoa wa Mbeya, Mhandisi Hamis Mrope, Mhandisi wa Miradi mkoa wa Rukwa na Katavi, Mhandisi Dunstan Kalugira.
Wengine ni Meneja wa Mradi wa REA III, Mzunguko wa Pili, Mhandisi Mustapha Himba, wengine ni Mwakilishi wa Menejimenti, Bwana Dude Fuime pamoja na Augustino Lyimo Msimamizi wa Mradi wote wanatoka kampuni ya ETDCO; kampuni inayojenga miundombinu ya Mradi huo.
Pamoja na kutembelea kijiji hicho na kujionea maendeleo ya Mradi huo; Viongozi hao walipata nafasi ya kuzungumza na Mwenyekiti wa kijiji hicho Bwana Richard Kalekene ambaye amewaeleza kuwa Wananchi wanasubiri kwa hamu kuunganishwa na huduma ya umeme na kuongea kuwa Kaya 18 zimeshafanya maandalizi ya usukaji (Wiring) kwa ajili ya kuunganishwa na nishati ya umeme.
“Wananchi wameupokea Mradi vizuri na wanahamu ya kuanza kutumia umeme, wanangoja kwa hamu siku ya kuwasha”. Alisema Mwenyekiti wa kijiji hicho, Bwana Kalekene.
Naye Mjumbe wa Bodi ya Nishati, Bwana Florian Haule amemweleza Mwenyekiti huyo kuwa ni muhimu Wananchi wakaendelea kuelimishwa kuhusu manufaa ya nishati ya umeme kwa kuwa lengo la Serikali katika kupeleka miradi hiyo n kuchochea maendeleo ya kiuchumi kwa Wananchi.
“Tuwasisitize na kuwaelimisha Wananchi wa hapa kuhusu umuhimu wa nishati ya umeme kwenye kuchochea maendeleo ya kiuchumi, mfano hapa Wananchi wengi ni Wakulima, jiandaeni kuanza kuongeza thamani ya mazao ya kilimo badala ya kuuza mahindi, zifungwe mashine za kusaga nafaka na muuze unga badala ya mahindi”. Alisema Mjumbe wa Bwana, Florian Haule.
Kwa upande wa Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi, Mhandisi Jones Olotu alisema, Serikali kupitia REA itaendelea kutekeleza miradi mingine kwa kuwa bado Wananchi wengi wanahitaji nishati ya umeme na nishati nyingine.
“Mwenyekiti, nafahamu unahitaji kila Mwanakijiji apate huduma ya umeme, Wateja wa awali 42 wataunganishwa lakini fursa bado zipo na Serikali inaleta miradi kwa kadili fedha zitavyopatikana, hii ni awamu moja, itakuja awamu nyengine, bado kuna mradi ya ujazilizi, ambao utaongeza wigo wa Wananchi wengi zaidi kufikiwa na huduma ya nishati ya umeme”. Alisisitiza Mhandisi Olotu.
Wakati huo huo, Meneja wa Mradi huo, Mhandisi Mustapha Humba amesema mbali na wilaya ya Mbeya vijijni kupata huduma hiyo wilaya ya Chunya, Kyela, Mbarali na Rungwe nazo zitanufaika kupitia Mradi wa REA III, Mzunguko wa Pili.
Kijiji cha Wimba kina wakazi zaidi ya 1,000 ambao wengi wa wanajishughulisha na kilimo cha zao la mahindi, maharage, pareto na mazao ya bustani kama vitunguu na parachichi.