Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akizungumza na Mzee Maduruki Nangeleke (kulia) mara baada ya kumaliza mkutano na wanachama wa Tawi la Kibaoni uliofanyika kwenye uwanja wa Kololo.
Katibu Mkuu ameongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndugu Sophia Mjema pamoja na Katibu wa NEC Oganaizesheni Ndugu Issa Haji (Gavu) kwenye ziara ya mkoa wa Morogoro yenye lengo kukagua, kusimamia na kuhimiza utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025 sambamba na kukagua uhai wa Chama.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akimsikiliza kwa makini Mbunge wa Jimbo la Mvomero Ndugu Jonas Van Zeeland wakati wa mkutano wa Shina namba 18, Mikoroshini kata ya Dakawa mkoani Morogoro.