Mfano wa hundi ya shs 100 milioni iliyotolewa na Nabii mkuu katika soko la Samunge lililopo jijini Arusha.
Mtume ,Balozi wa Nabii mkuu Mh Dkt GeorDavie wa kanisa la Ngurumo ya upako Sekela Ntondolo akizungumza kwa niaba ya Nabii mkuu wakati wa kukabithi hundi hiyo katika soko la Samunge jijini Arusha.
………………………………………….
Julieth Lazier,Arusha .
Nabii mkuu Dkt GeorDavie wa kanisa la Ngurumo ya upako leo amekabithi rasmi hundi ya shs 100 milioni kwa soko la Samunge fedha alizoahidi hivi karibuni kwa ajili ya ukarabati na kuwasaidia wajasiriliamali wenye mitaji midogo katika soko la Samunge lililopo kata ya mjini kati mkoani Arusha.
Akikabithi rasmi hundi hiyo leo kwa niaba ya Nabii huyo katika soko la Samunge ,Mtume Balozi wa Nabii mkuu Mh.Dkt GeorDavie ,Sekela Rowland Ntondolo amesema kuwa, Nabii GeorDavie ni msikivu na ni mtu wa watu hivyo ametekeleza kile alichoahidi kwa vitendo ikiwa ni sehemu mojawapo ya kumuunga mkono Rais Samia katika kuchangia shughuli mbalimbali za maendeleo.
Aidha katika ahadi yake,Nabii alisema kuwa,kiasi cha shs milioni 80 watagawiwa mtaji wajasiriamali wenye mitaji midogo na huku shs milioni 20 ikitumika kwa ajili ya kukaratabati soko hilo.
Balozi Ntondolo amesema kuwa,watu wengi huvunja biashara zao kwa maneno yao wenyewe badala yake amewataka subiri maneno ya ushindi katika biashara zao ili ziweze kubarikiwa na kuendelea kukua zaidi.
“Mnatakiwa mzungumze maneno mazuri tena kwa ujasiri mkubwa kuhusu biashara zenu na kupitia fedha hizi mkafanye biashara kwa bidii huku mkimwomba Mungu mfaidi matunda ya fedha hizo mlizopewa na Nabii “amesema Mtume Balozi Ntondolo.
Mwenyekiti wa wafanyabiashara wa soko hilo Njola Miraji, amemshukuru nabii mkuu kwa kutimiza ahadi yake akidai kuwa wapo mabilionea waliotokana na madini ya Tanzanite lakini wameshindwa kusaidia jamii yenye uhitaji .
Amesema katika fedha hizo wameorodhesha majina ya wafanyabiashara 1261watakaonufaika na fedha hizo na tayari majina hayo ameyakabidhi kwa nabii mkuu kama alivyoelekeza wakati akiajidi fedha hizo .
Naye mkuu wa soko hilo,Restituta Nyoni amewataka wafanyabiashara watakaonufaika na fedha hizo kuzielekeza kwenye biashara husika na kuepuka kuzipeleka mambo yasiofaa ikiwemo kwenye vikoba.
“Endapo utapokea hizo fedha nenda kafanye biashara usiende kunywea pombe au kuingiza kwenye vikoba”amesema Nyoni.