MWENYEKITI wa Baraza la Ushindini (FCT) Mhe.Salma Maghimbi,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kwenye banda la FCT wakati wa Maadhimisho ya wiki ya Sheria yanayoendelea jijini Dodoma.
MSAJILI wa Baraza la Ushindani (FCT)Mhe.Renatus Rutatinisibwa ,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kwenye banda la FCT wakati wa Maadhimisho ya wiki ya Sheria yanayoendelea jijini Dodoma.
……………………………………..
Na Mwandishi Wetu-DODOMA
BARAZA la Ushindani (FCT) limewataka wananchi kutumia vyombo vya udhibiti ambavyo vipo na vimeundwa kwa ajili yao lengo likiwa ni kutatua migogoro na kutenda haki .
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Baraza la Ushindini (FCT) Mhe.Salma Maghimbi, wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye banda la FCT wakati wa Maadhimisho ya wiki ya Sheria nchini yanayoendelea jijini Dodoma.
Mhe.Maghimbi amesema kuwa wananchi wamekuwa na malalamiko bila kujua wapi pa kwenda kupekeka.
“Kwa mfano watu wanatumia huduma Kama vile Mawasiliano ,maji Mafuta na vitu vingine kama wamekuwa na shida, wanamalalamiko na kutokujua waende wapi vyombo husika Baraza la Ushindani lipo katika kuleta haki
Na kuongeza ” Hivyo niwatake wananchi wasikate tamaa wanapoona msuala yao hayamalizika vizuri ,”amesema
Aidha akielezea kuhusu kuanzisha kwa Baraza la Ushindani amesema Baraza hilo liliundwa baadaa ya nchi yetu kutoka kwenye uchumi Hodhi na kuingia kwenye uchumi wa soko.
Amesema baada ya kuonekana maeneo mbalimbali ya kiuchumi ambayo hayawezi kuachiwa kwenda kwenye uchumi wa soko lakini lazima viundwe Chombo vya kudhibiti zile sekta za kiuchumi ili ziweze kufanya ushindani katika biashara ziwe za haki.
Mfano kwenye suala ya mafuta petrol, umeme ndio yakaundwa mbaraza ya udhibiti kutokana na asili na shughuli zinazofanywa kwenye zile sekta na kuwepo na hatari ya kupanda kwa bei .
Amesema Maamla hizo zilizoundwa zilipewa mamlaka ya kufanya maamuzi kutokana na Masuala yote yanayotokana na eneo yote zinazo dhibti au inaratibu waliopewa mamalaka ya udhibiti au tume ya ushindani.
Pia mamlaka hizo zimepewa mamlaka ya kufanya maamuzi kwenye migogoro mbalimbali na Masuala mbalimbali yanayousiana na sekta zao.
Naye Msajili Baraza la Ushindani (FCT) Renatus Rutatinisibwa amewataka wananchi watambue chombo hicho kipo kwaajili ya kuwahudumia hivyo kuacha tabia ya kukalia matatizo waliokuwa nayo baraza la Ushindani lipo na wanatoa haki .
Hata hivyo amezitaja Kesi walizo zipokea kutoka kwenye baadhi ya sekta nipamoja na EWURA 164 TCRA 102 FCC kesi 105 huku akisema Kwanini Ewura wako juu kwa kesi ni kutokana na kuhudumia sekta ngingi.