Afisa Mahusiano wa Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL) Edmond Rutajama akizungumza kwenye kikao kazi na wanahabari Mwanza
Meli ya Mv Mwanza Hapa kazi tu inayoendelea kujengwa katika Bandari ya Mwanza Kusini ambayo itagharimu kiasi cha shilingi billion 108
Viongozi wa Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL) wakiwa kwenye kikao
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa MSCL
…………………………………
Na Hellen Mtereko, Mwanza
Kampuni ya Huduma za Meli Nchini (MSCL) inatekeleza miradi 12 yenye thamani ya sh Billion 113 Kwa mwaka wa fedha 2022/ 2023.
Hayo yamebainishwa Jana Januari 25,2023 na Afisa Mahusiano wa (MSCL) Edmond Rutajama, katika kikao kazi na waandishi wa habari wa Mkoa wa Mwanza.
Rutajama ameeleza kuwa miradi 7 itakayo gharimu kiasi cha Sh, Billion 53 itakuwa katika Ziwa Tanganyika na miradi 5 itagharimu kiasi cha Sh Billion 57 Mkoani Mwanza na sh Billion 2 zitatumika kuendesha Meli walizopewa na Mamlaka ya Bandari.
Amefafanua kuwa kutokana na fedha hizo walizopewa zitagawanywa katika miradi minne (4) ambayo ni Mipya Miradi Mitano (5) ambayo ni ya ukarabati na mingine mitatu (3) inayoendelea kutekelezwa na Kampuni hiyo ikiwemo, Ujenzi wa Meli ya Mv Mwanza hapa Kazi tu inayojengwa.
Rutajama ameeleza kuwa meli hiyo ya Mv Mwanza hapa kazi tu itagharimu kiasi Cha Bil 108 mpaka kukamilika ambapo mpaka sasa imefika asilimia 80 tangu kuanzwa kutengeneza kwake.
” Meli hii ya Mv Mwanza Hapa kazi tu ni meli kubwa kuliko Meli zote katika ukanda wa maziwa makuu, ni meli ambayo imetuheshimisha wananchi na serikali Kwa ujumla”alisema Rutajama.
Aidha wamemshukru Rais Dkt Samia Kwa kuendelea kutenga fedha na kuifanya kampuni hiyo kuendelea kusimama na kutimiza malengo.