NA EMMANUEL  MBATILO, DAR ES SALAAM

BARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) wamesaini mkataba wa miaka mitatu wa ushirikiano na Taasisi inayojishughulisha na masuala ya kisayansi na kimazingira kutoka  nchini India ambapo  ushirikiano huo utasaidia kufanya maboresho katika ukusanyaji  wa taka ngumu.

Akizungumza na waandishi  wa habari leo Januari 23,2023 Jijini Dar es Salaam,  Mkurugenzi wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Dkt. Samuel Gwamaka amesema NEMC pamoja na Center for  Science and Environment wamekusudia kujengeana uwezo na uzoefu kuwa pamoja na kufanya tafiti zinazohusiana na miji  yetu katika ukusanyaji  taka lakini vilevilekubadilishana uzoefu ambapo  baadhi ya wataalamu  wao wanaweza kupewa mafunzo.

  Amesema nia ya mkataba huo uwe wa miaka mitatu kuanzia sasa lakini  kutakuwa na uwezekano kuupeleka mbele zaidi lengo kubwa ni kuzipa nguvu Mamlaka za Serikali za Mitaa hasa katika majiji, miji  pamoja  na Wilaya ndo  maana wakurugenzi wameweza kushiriki  kwenye mkutano huo ili  waweze kubadilishana mawazo  na uzoefu ili baadae tuwe na mifumo  ya kisasa kuhakikisha taka ngumu zinazozalishwa ziwezwe kutengwa na zisionekane kwenye madampona zile zinazooza ziweze kuwa mbolea.

“Suala la taka ngumu limekuwa changamoto katika  miji mingi sio Tanzania tu,lakini katikanchi mbalimbali kwahiyo tumekuwa na wenzetu kutoka nchi mbalimbali ikiwemo Rwanda, Kenya, Uganda, Ethiopia, Eswatini, Ghana , Zambia ambao na wao wametuma wawakilishai  wao hapa kuja kujadili na kuweza kubadilishana uzoefu”. Amesema 

Aidha amesema madampo imekuwa mojawapo ya sehemu ambayo ni  changamoto na ni gharama katika  kuyaendesha katika  uksanyaji wa taka  ngumu  na matokeo yake miji  yetu mingi  imekuwa ni michafu  hivyo kupitia Taasisi hiyo kutoka India ambao wao wamekwenda mbali katika teknolojia hivyo kusaidia kutengeneza mifumo rafiki kwaajili  ya kutenga taka ngumu zisiweze kuleta madhara kwenye mazingira.

Kwa upande wake Mwakilishi kutoka OR TAMISEMI, Bi.Hawa Mwechaga amesema TAMISEMI inasimamia halmashauri 184 ambako huko  kote kuna taka ngumu kwahiyo kwa kila halmashauri wana idara zinazoratibu uzalishaji wa taka ngumu hivyo wanashirikiana na NEMC kuona ni namna gani wanaenda kuboresha Majiji na miundombinu mbalimbali.