Afisa Mfawizi Latra Halima Lutavi akizungumza na waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda kabla ya kuwagawia vitambulisho
Mwenyekiti wa chama Cha Mwapita Makoye Kayanda
Afisa Mfawidhi LATRA Halima Lutavi akigawa vitambulisho kwa waendesha bodaboda
Waendesha bodaboda wakiwa kwenye picha ya pamoja
****************************
Na Hellen Mtereko, Mwanza
Chama ha waendesha Pikipiki Mkoa wa Mwanza Mwapita kimetoa vitambulisho Kwa wananchama wake vitakavyowasaidia kuwatambulisha mahala pa kazi na pindi wanapofikwa na matatizo.
Mwenyekiti wa chama hicho Makoe Kayanda ameeleza kuwa lengo la kutengeneza vitambulisho hivyo na kuvigawa ni kuhakikisha mwanachama anapohitaji msaada wowote kwenye chama au jamii anapata Kwa urahisi Kwa kuwa wanamtambua.
“Vitambulisho vitawasidia pindi mtu anakuwa amepatwa na tatizo katika kazi zake na kitambulisho hicho kitaweza kumsaidia kupata msaada Kwa kutoa taarifa sehemu husika” Alisema Kayanda.
Kayanda ameeleza kuwa Ili mwanachama aweze kupatiwa huduma ni lazima awe na kitambulisho kinachomtambulisha kuwa mwanachama wa chama hicho pamoja na kuwataka waendesha pikipiki na wasio waendesha pikipiki kujiunga kwani chama hicho ni Kwa ajili ya watu wote na sio waendesha boda boda peke yao.
Halima Lutavi ni Afisa Mfawizi Latra ameeleza kuwa vitambulisho hivyo ni muhimu boda boda hao kuwa navyo kwani vitawasaidia Kwa sehemu kubwa pindi mtu anapofikwa na tatizo hususani kipindi ambacho yuko nje ya kituo chake cha kazi.
” Ikitokea mtu amepata tatizo alafu yuko mbali na kituo chake kulingana na utandawazi uliopo Kwa sasa anaweza kupata msaada kiurahisi pindi nyaraka zake za kitambulisho zinapoingizwa kwenye mtando Kwa kutumia kitambulisho alichokuwa nacho” alisema Halima.
Hata vivyo ameeleza kuwa vitambulisho hivyo vitawasidia wao kama Latra kupata takwimu sahihi za waendesha boda boda Mkoa wa Mwanza.
Kwa upande mwingine amewataka waendesha boda boda kukaa katika maegesho na maeneo ambayo ni salama kwa kazi zao na kuachana na tabia ya kukaa sehemu ni hatarishi kwao.
” Unakuta mtu amekaa kwenye Kona au chini ya transifoma sehemu ambayo ni hatarishi kwenye maisha yake, ni lazima mjaribu kufikilia nafsi zenu kwanza sio Kila sehemu mnakaa kama hauna sehemu maalumu ya maegesho nenda sehemu husika utapangiwa eneo.
George Masake ni mmoja wa wendesha boda boda aliyepata kitambulisho ameeleza kuwa vitambulisho hivyo vitawasidia Kwa sehemu kubwa wawapo katika kazi zao, hususani linapotokea tatizo.
” Vitambulisho hivi vitatusaidia Kwa sababu sisi boda boda tunaenda maeneo mbalimbali kufanya kazi hivyo vitakuwa ni sehemu yetu ya utambuzi pindi tunapokuwa tunatekeleza majukumu yetu.