Nabii Mkuu Dkt.Georgdavie akizungumza na wananchi wa soko la Samunge jijini Arusha leo .
Mbunge wa Arusha mjini,Mrisho Gambo akizungumza na wananchi katika soko la Samunge jijini Arusha.
Wananchi mbalimbali wakimsikiliza Nabii Mkuu Dkt Geordavie wakati alipotembelea soko la Samunge kwa lengo la kuwawezesha wajasiriamali wenye mitaji midogo ili kuweza kukuza biashara zao na kujikwamua kiuchumi.
……………………………
Julieth Laizer ,Arusha.
Arusha.Nabii mkuu Dkt Geordavie wa kanisa la Ngurumo ya upako amekabithi hundi ya shs 100 milioni kwa ajili ya ukarabati na kuwasaidia wajasiriamali wenye mitaji midogo katika soko la Samunge lililopo kata ya mjini kati mkoani Arusha.
Akikabithi hundi hiyo leo jijini Arusha katika soko la Samunge ,Nabii amesema kuwa amewiwa kufanya hivyo baada ya kupata barua aliyoandikiwa ya kuhitaji msaada kwa ajili ya kukarabati na kusaidia wajasiriamali wenye mitaji midogo katika soko hilo ili waweze kujikwamua kiuchumi.
Amesema kuwa,kiasi cha shs milioni 80 watagawiwa mtaji wajasiriamali wenye mitaji midogo na huku shs milioni 20 ikitumika kwa ajili ya kukaratabati soko hilo.
“Mimi huu msaada ninatoa sitafuti waumini sipo hapa kumbadilisha mtu dini nipo hapa kuwasaidia wananchi katika kuondokana na changamoto mbalimbali
na asanteni sana kwa mabango na picha haya ni mahaba makubwa sana na asanteni kwa heshima yenu ya kunipa kuwa mlezi wa soko ila mniwie radhi tutakuwa tunashirikiana popote mnapohitaji msaada ila swala la kuwa mlezi sitaweza maana nina majukumu mengi sana”amesema Nabii.
Amesema kuwa,kinamsukuma kusaidia jamii ni Mungu alimwambia afanye injili kwa matendo kwani alishafanya injili kwa maneno sasa ni maneno machache kazi kubwa zaidi.
Aidha ametoa wito kwa Viongozi wa dini kutochukua sadaka tu wakati umefika wa kuanza kurudisha kile wanachokipata kwa wananchi ,ni wakati sasa turudishe fadhila kwa jamii tuwasaidie maana watu wanateseka ,tujitahidi kusaidia .
“Msaada huu nilioutoa ni baada ya kupokea barua yenu ya kuomba msaada na nimekuja kuwaunga mkono na kila mmoja anapaswa kutambua kuwa tunaposaidia jamii tutakuwa tumemsaidia pia Rais Samia Suluhu Hassan katika swala la maendeleo. “amesema.
Naye Mbunge wa Arusha mjini,Mrisho Gambo amesema kuwa,kazi ya viongozi wa serikali ni kuwaheshimu viongozi wote wa dini na kuwapa heshima yao pamoja na kuheshimu kipawa walichopatiwa.
Gambo amesema kuwa, mnamo mwaka 2019 soko liliungua kwa moto na tangu lilipoungua walijisaidia wenyewe na wameendelea kuishi kwenye changamoto hiyo kwa muda mrefu.
“Hapa soko la Samunge tunakabiliwa na changamoto ya ukarabati wa soko kwani mvua ikinyesha matope na mvua ni ya kwao ,sambamba na usumbufu mkubwa wa mgambo wanaoupata sokoni hapo.”amesema.
Amesema kuwa ,amewahi kutoa kiasi cha shs milioni 20 kama mtaji kwa wanawake wa soko hilo kwa ajili ya kuwasaidia wanawake kuondokana na changamoto mbalimbali.”amesema.
Gambo amesema kuwa , katika kuhakikisha anasaidia ukarabati wa soko hilo anatoa kiasi cha shs Milioni 10 .
Amefafanua kuwa,Rais Samia ameonyesha njia tayari na anaenda kujenga soko la kisasa kilombero na kwa mrombo pia .
Diwani wa kata ya Mjini kati, Abdulrasul Tojo amesema kuwa , wanaenda kuweka historia kwa kujenga hoja baraza la madiwani ili soko hili liwe chini yake.
Aidha Diwani huyo walimwomba Dokta Nabii Georgdavie kuwa soko hili liwe chini yake kwani tangu lilipo ungua limekuwa katika hali ya mbaya hadi sasa hivi.
Akisoma risala kwa niaba Wafanyabishara wa soko la Samunge,Loveless Joakim amesema kuwa,soko la NMC lilianzishwa mwaka 2012 kwa lengo kusaidia wafanyabiashara wapo katika soko hilo waliopo 2,106 .
Amesema kuwa, walipata changamoto kuunguliwa na soko hilo mwaka 2019 na baada ya hapo moundombinu mingi iliharibika na kupelekea kila mmoja kujijengea soko na mahitaji mengine huku bado wakiendelea na changamoto hiyo.