Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Mh.Aziza Mangosongo Tarehe 19/01/2023 akiwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Nyasa, ametembelea na kukagua miradi (2) ya maendeleo,ya Ujenzi wa Barabara za Mitaa katika Mji wa Kitalii wa Mbamba bay, na Mradi wa Ujenzi wa Ofisi ya Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Wilayani Nyasa.
Akikagua Mradi wa Ujenzi wa barabaraza mitaa katika Mji wa kitalii wa Mbamba bay, wa kiwango cha Lami Mh. Mangosongo amesema ameridhishwa na kazi ya ujenzi wa barabara hizo, baada ya kukuta ujenzi uko asilimia 70 na Mkandarasi yuko kazini akitekeleza majukumu yakena kuipongeza TARURA kwa Utekelezaji wa miradi bora ya barabara Wilayani Nyasa.
Amewataka wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) Wilayani Nyasa kuendelea kumsimamia mkandarasi, anayetekeleza Mradi ili aweze kukamilisha kwa muda uliopangwa.
Awali akitoa Taarifa ya Mradi wa Ujenzi wa Barabara za mitaa katika Mji Mkongwe wa Mbamba bay Wilayani Nyasa, Meneja wa TARURA Wilayani Nyasa Mhandisi Thomas Kitusi amesema, Mradi wa Ujenzi wa Barabara za mitaaa Mbamba bay utagharimu Tsh Milionio 500 ambazo zimetolewa na Serikalika kupitia Mfuko wa Jimbo.
Aidha Mradi huu unajenga barabara za Mitaa ,Mbamba bay kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya barabara ili watalii wanavyofika waweze kuvutiwa na Mji wa Mbamba bay.
Mradi huu ni wa Km. 01 na unatarajia kukamilika Mwezi Februari 2023 Mwaka Huu na kukamilika kwa barabara za Mitaa katika mji wa Mbamba bay kutatatua changamoto ya ukosefu wa barabara katoika mji huo.
Katika Ujenzi wa Ofisi ya TAKUKURU wilayani Nyasa iliyofikia hatua ya msingi, Mkuu huyo ameipongeza Ofisi kwa kujenga Ofisi katika Wilaya ya Nyasa na kusema kuwa kukamilika kwa ofisi hiyo kutapunguza malalamiko ya wananchi, na uendeshaji wa ofisi kwa kuwa kwa sasa hawana jengo la Ofisi.
Awali akitoa Taarifa ya Ujenzi Kamanda wa TAKUKURU Wilayani Nyasa Dioniz Slivanus amesema Mradi uko ngazi ya Msingi, na kukamilika kwa Ujenzi wa Ofisi kunatarajia kutatua kero ya ukosefu wa Ofisi ya TAKUKURU Wilayani Nyasa.