MWENYEKITI wa CCM Mkoa wa Tanga Rajabu Abdurhaman akizungumza na wazee wa Mkoa wa Tanga |
MWENYEKITI wa CCM Mkoa wa Tanga Rajabu Abdurhaman akizungumza na wazee wa Mkoa wa Tanga |
MWENYEKITI wa CCM Mkoa wa Tanga Rajabu Abdurhaman akizungumza na wazee wa Mkoa wa Tanga |
Sehemu ya Wazee wa Mkoa wa Tanga wakifuatilia matukio mbalimbali
Na Oscar Assenga, TANGA.
MWENYEKITI
wa CCM Mkoa wa Tanga Rajabu Abdurhaman amesema wamejipanga ndani ya
miaka mitano ya uongozi wao kuhakikisha wanaurudisha mkoa huu kwenye
hadhi yake ya viwanda kwa kuvutia wawekezaji wapya.
Mkakati huo
ulitangazwa na Mwenyekiti huyo wakati wa kikao chake na Wazee wa Mkoa wa
Tanga kilichofanyika kwenye ukumbi wa CCM Mkoa wa Tanga ambapo alisema
watakachofanya ni kuanisha viwanda vilivyopo kuona changamoto zao na
kuona namna ya kuzipatia ufumbuzi.
Rajabu alisema pamoja na hayo
ni kuona namna bora ya kuwavutia wawekezaji wapya kwenda kuwekeza
kwenye mkoa Tanga ambao una fursa nyingi za kiuchumi ambazo
zitawawezesha kuendesha shughuli zao bila vikwazo.
“Kama Mkoa wa
Pwani wameweza kufanya vizuri kwenye viwanda kwanini Tanga ambako ndio
kwenye asili ya viwanda nyie wazee wetu ndio mnaijua hii vizuri
tuiteni mtueeleza kwamba tunakosea wapi moja mbili tatu wazee wetu
mnafahamu ”Alisema
“Bandari ya Tanga ilifanya kazi ipasavyo,Reli
na tukawa na viwanda vya kutosha ajira za kumwaga na tukachangia kwa
kiasi kikubwa pato la uchumi wa Taifa letu lakini niwaambie kwamba kwa
sasa tumedhamiria kuirudisha Tanga kwenye hadhi yake tena kwa haraka
sana ”Alisema Mwenyekiti huyo
Hata hivyo alisema kwamba uchumi
wa Tanga ukiinuka hata vilabu vya Coastal Union na African Sports navyo
vitainuka kwa sababu watu wataweze kuvichangia vilabu vyao.
Kuhusu Migogoro ya Ardhi
Mwenyekiti
huyo alisema kwamba wamejipanga vema kwa kushirikiana na Mkuu wa Mkoa
wa Tanga Omari Mgumba kukaa chini kutafutaka namna bora na nzuri ya
kuweza kuondoa migogoro ya ardhi kwenye mkoa huo.
Rajabu alisema
unaweza usione athari ya migogoro ya ardhi baina ya wakulima na
wafugaji mpaka pale utakapopigiwa simu kwamba ndugu yao ameuwawa
kutokana na migogoro ya ardhi kwenye maeneo yao.
“Tumeenda
wenyewe kwenye baadhi ya maeneo hatukutaka kusimuliwa watu imefika
wakati wakulima na wafujaji wanauana wanachomea mali zao ukikaa mjini
yanayoendelea vijijini huwezi kuyajua na mimi niliomba Uenyekiti kuja
kusaidia chama changu,wananchi wa Tanga tumeenda kujioneka na baadhi ya
maeneo hali sio shwari lakini kwa kufika CCM katika maeneo hayo hali
nzuri imerejea na shwari watu wanaishi kwa Amani hivyo tuitake jamii
iendelee kuienzi Amani iliyopo”Alisema
Hata hivyo alisema kwamba
wanajua serikali inadhamira njema na mkoa wa Tanga na Rais Samia kwa
hatua kubwa anayoendelea kuichukua kuimarisha Tanga kiasiasa na kiuchumi
hivyo aliwataka waendelee kumpa muda Rais ikiwemo kumuombea na
kumuunga mkono yeye na Makamu wa Rais Philip Mpango,Waziri Mkuu Kasim
Majaliwa.
Kauli yake kwa viongozi wa dini.
Mwenyekiti
huyo aliwataka viongozi wa dini na wazee wa mkoa huu waisaidie Serikali
katika suala la mmomonyoko wa maadili ambalo limekuwa ni tatizo .
“Hivyo
tukirudi kwenye maadili mazuri nchi yetu itaendelea kuwa salama na
lawama kwa serikali itaondoka na kupungua kwa asilimia kubwa hivyo suala
hilo ni muhimu mkubwa kwenu kuhimiza maadili mema “Alisema
Katibu
wa CCM Mkoa wa Tanga Suleiman Mzee alisema Mwenyekti baada ya
kuchaguliwa alianza kazi za dharura ikiwemo ya maeneo yalikuwa migogoro
ya ardhi mikubwa baina ya wakulima na wafugaji nako kumeanza kutulia.
Alisema sasa wanataka kuanza rasmi kazi za Chama wakaona sio vema kuanza
bila kukutana na wazee wa mkoa huo wafanye kikao hicho kwa ajili ya
Baraka kwa ajili ya ratiba zao mbalimbali za kichama.