Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekoutoure Bahati Msaki akizungumzia bima ya afya kwa wote itakavyorahisisha upatikanaji wa matibabu.
Meneja wa mfuko wa Taifa wa bima ya afya (NHIF) Mkoa wa Mwanza Emmanuel Mwikwabe
Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dkt Silas Wambura (wakwanza kulia)akizungumzia umuhimu wa Wananchi kuwa na bima ya afya
…………………………….
Na Hellen Mtereko,Mwanza
Sheria inayopendekezwa na Waziri mwenye dhamana ya masuala ya afya, bima Kwa wote ikiwa na lengo la kuweka utaratibu utakaowasaidia watanzania wote kupata huduma za kimatibabu Kwa urahisi zaidi.
Meneja wa Mfuko wa Taifa bima ya afya (NHIF) Mkoa wa Mwanza Emmanuel Mwikwabe, amesema kuwa muswada wa bima ya afya Kwa wote utajumuisha watanzania wengi zaidi kupata matibabu bora.
Mwikwabe amesema kuwa bima hiyo itazingatia viwango ambavyo wananchi wanauwezo wa kuvimudu na kuweza kuchangia ili wanapokwenda vituo vya afya waweze kupatiwa matibabu Kwa kupitia bima na sio kutoa fedha taslimu.
” Maana sio wakati wote mtu unaweza kuwa na fedha za kugharamia matibabu anapokuwa ameugua ila ukiwa na bima ya afya itakuwa msaada mkubwa unapopatwa na maradhi” alisema Mwikwabe.
Amesema kuwa takribani asilimia 85 ya Watanzania hawako kwenye Mfumo wa bima ya afya kutokana na changamoto mbalimbali ambazo Kwa namna moja ama nyingine zinakuwa sababu ya wao kushindwa kujiunga na bima hiyo.
Mwikwabe amesema kuwa kupitia utaratibu huo wananchi wanapaswa kujiunga na huduma hiyo na kupelekea kupata huduma za matibabu kuboreshwa zaidi,na Kwa makundi ambayo hayana uwezo wa kulipia gharama za matibabu watakuwa wametengenezewa mazingira rafiki ya kupata matibabu na kuondokana na Watanzania ambao wanakwenda kwenye vituo vya matibabu na kushindwa kulipa gharama.
Mganga Mfawizi Hospital ya rufaa Mkoa wa Mwanza Sekoutoure Bahati Msaki, ameeleza kuwa bima ya afya Kwa wote itakuwa na manufaa Kwa kundi kubwa la wananchi na wataweza kupata huduma ya matibabu Kwa urahisi.
Msaki ameeleza kuwa wanahitaji kupata asilimia 100% ya Watanzania watakaijiunga na bima ya afya kwani bima hiyo itasaidia kuboresha huduma katika hospital,kuongeza kipato Kwa mwananchi mmoja mmoja.
” Na Kila mwananchi akiwa na afya njema ataweza kufanya kazi vizuri na kuboresha maisha, hivyo sisi Kama watumishi wa sekta ya afya tunaunga huduma ya bima ya afya Kwa wote” alisema Msaki.
Kwa upande wake Dokta Sailas Wambura Kaimu Mganga mkuu wa Mkoa wa Mwanza amesema kuwa Kupitia Sheria inayopendekezwa, watu wasio na uwezo watakuwa na haki ya kupata huduma za matibabu kupitia utaratibu uliowekwa na Serikali baada ya kuwatambua kupitia mfumo wa utambuzi wa watu wasio na uwezo.
Wambura ameeleza kuwa Ili kuhakikisha uhai na uendelevu wa Mfuko, wakati wa utekelezaji wa sheria ya bima ya afya kwa wote, wanufaika wa bima ya afya watatakiwa kufuata utaratibu wa rufaa wakati wa kupata huduma
za matibabu kuanzia ngazi ya Zahanati hadi Hospitali ya Taifa.
Aidha amewataka watanzania kuhakikisha wanajiunga na bima ya afya Kwa wote ili wawe wanapata huduma kwa urahisi na kuachana na utaratibu wa kukata bima wanapofikwa na maradhi.