James manjara mfugaji anae simamia mifugo ya Baba yake Michael Lusomi akiwa
Baadhi ya Ng’ombe anaowafuga James Manjara
Wakwanza (kulia) ni mtafiti wa mifugo kutuko taasisi ya utafiti wa mifugo Taliri Godfrey Chasama akiwa na James manjara ambae ni mfugaji
**************************
Na Hellen Mtereko, Mwanza
Wafugaji wameshauriwa kutumia madume ya Ankole na Ng’ombe wa kienyeji kwaajili ya uzalishaji kwani ni mfumo mzuri utakao wasaidia kuwa na ufugaji wenye tija.
Ushauri huo ulitolewa Jana Januari 17, 2023 na Mtafiti wa mifugo Godfrey Chasama, kutuko taasisi ya utafiti wa mifugo Tarili kituo cha Mabuki kilichopo Wilaya ya Misungwi Jijini Mwanza.
Alisema kuwa wafugaji wengi bado wanafuga kijadi hali inayopelekea kuona ufugaji wao hauna tija,aliongeza kuwa moja ya shughuli ambazo wamefanya kwa kipindi kirefu chini ya utafiti huo kwenye idara ya Ng’ombe ni kuboresha uwezo wa Ng’ombe kiuzalishaji ambao kiutaalam unaitwa (BLEEDING).
Chasama alieleza kuwa mwaka 2012 walianzisha utaratibu wa kupanga kitu na wafugaji ambao wanafikika kirahisi katika maeneo ya jirani kulingana na Ng’ombe waliopo(outreach program) ambayo ililenga kuboresha Ng’ombe wa Zibu aina za Kisukuma na Tarime kwakutumia aina ya Ankole ambae kiuzalishaji ana ubora mkubwa ukilinganisha na Zibu.
Alisema kuwa wanafanya kazi ya kuzalisha mbegu kwakufanya tathimini ya wanyama tangu anapozaliwa anachukuliwa uzito,anapoachishwa kunyonya anachukuliwa uzito na anapotimiza mwaka mmoja anachukuliwa uzito,mwisho wanaangalia vigezo vya kuwachagua ambao wako kwenye asilimia 60 wanakuwa na ubora wa kusambazwa Kama mbegu kwa wafugaji ambao wanahusishwa kwenye outreach program.
“Matokeo ya ufugaji yalikuwa ni mazuri kwani Ng’ombe walikuwa wanazaliwa na wanakuwa vizuri na mfugaji anatafutwa sana na wanunuaji wa Ng’ombe na hata akienda mnadani anakuwa na uhakika wa kuuza”,alisema Chasama
Kwa upande wake Mtoto wa Michael Lusomi anaesimamia shughuli zote za ufugaji wa Ng’ombe James Manjara alisema kuwa walianza ufugaji wa mchanganyiko baada ya kupewa elimu na watafiti kutoka Taasisi ya Taliri.
“Tulipewa elimu ya ufugaji wa kutumia mfumo wa madume ya Ankole na Ng’ombe wa kienyeji,tulianza ufugaji huo wa mchanganyiko ambao umetuletea mabadiliko makubwa sana ukilinganisha na ufugaji wa zamani”,alisema Manjara
Alisema kuwa pamoja na changamoto wanazopitia ikiwemo magojwa na malisho bado wanajitahidi sana kukabiliana nazo ili kuweza kuwakomboa.
Manjara aliongeza kuwa mwanzoni walikuwa wakiuza Ng’ombe wa kienyeji wa miaka 2 kwa laki 2 lakini kwa sasa Ng’ombe wa miaka miwili wanauza laki 5 hadi 7 hivyo utofauti ni mkubwa sana Kati ya Ng’ombe wa kienyeji na hawa wa mchanganyiko.
Alieleza kuwa kwaupande wa maziwa pia kunautofauti mkubwa kwani Ng’ombe mmoja wa mchanganyiko ukimkamua unapata lita moja na nusu au mbili za maziwa lakini wa kienyeji walikuwa wanapata robo lita.
Mwisho alitoa wito kwa wafugaji wengine ambao hawajaanza ufugaji wa mchanganyiko wajitokeze wapate elimu ili waweze kufuga ufugaji huo wenye tija utakaoweza kuwatimizia mahitaji yao Kama ilivyo kwao inavyowasaidia katika shida mbalimbali ikiwemo kulipa ada.