Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Dkt. Ibrahim Isack akizungumza kwenyeuzinduzi wa mfumo wa m-mama leo mjini Sumbawanga amesema wataratibu mkutano wa watendaji wa vituo vya afya ili kuwakumbusha umuhimu wa kuboresha huduma kwa wateja ,maadili na matumizi ya lugha nzuri ili wanacnchi wanufaike na mfumo huo wa mawasiliano hatua itakayosaidia kupunguza vifo vya wajawazito.
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Donald Nssoko amewapongeza wadau wa maendeleo ikiwemo Vodacom/Vodafone na washirika wake Touch Foundation na Pathfinder International kwa kushirikiana na serikali kutekeleza mfumo wa m-mama utakaosaidia kupunguza vifo vya wajawazito na watoto.
Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Sebastian Waryuba akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo Queen Sendiga leo kwenye uzinduzi wa mfumo wa m-mama unaolenga kutoa huduma za dharura za usafiri kwa wajawazito kufikia vituo vya kutolea huduma.
Mratibu wa Huduma za Afya ya Mama na Mtoto Mkoa wa Rukwa Asha Ressa Izina amesema katika kipindi cha miaka mitano (2018-2022) jumla ya vifo 274 vya akina mama wajawazito vilitokea huku vizazi hai vikiwa ni 277,987 hivyo kuhitajika mkakati maalum kuvimaliza ikiwemo mfumo wa m-mama.
Viongozi wa mkoa na wilaya walioshiriki uzinduzi wa mfumo wa m-mama leo mjni Sumbawanga wakifuatilia mada za kikao.
Mratibu wa Huduma ya Afya ya Mama na Mtoto OR-Tamisemi Dkt. Yahaya Hussein akizungumza leo mjini Sumbawanga amesema mfumo wa m-mama ulianza mwaka 2013 na sasa unatekelezwa katika mikoa mitano huku lengo ni kufikia mikoa yote kama Rais Samia Suluhu Hassan alivyoagiza.
(Habari na Picha na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa)