Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akishiriki Ibada ya kawaida ya katikati ya juma katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Karoli Lwanga Jimbo Katoliki la Kahama leo tarehe 18 Januari 2023.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akizungumza na waumini mara baada ya kushiriki Ibada ya kawaida ya katikati ya juma katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Karoli Lwanga Jimbo Katoliki la Kahama leo tarehe 18 Januari 2023.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja na Askofu wa Jimbo Katoliki la Kahama Christopher Ndizeye (Wa pili kutoka kulia) pamoja na Mapadre na watumishi wa kanisa mara baada ya kushiriki Ibada ya kawaida ya katikati ya juma katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Karoli Lwanga Jimbo Katoliki la Kahama leo tarehe 18 Januari 2023.
………………………………….
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango ametoa wito wa waumini na watanzania kwa ujumla kuhakikisha wanatenda na kusimamia haki katika Maisha yao ya kila siku husasani kwa wananchi wanyonge ili kuwa na taifa lenye umoja na amani.
Makamu wa Rais amesema hayo mara baada ya kushiriki ibada ya kawaida ya katikati ya juma katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Karoli Lwanga Jimbo Katoliki la Kahama leo tarehe 18 Januari 2023, ibada iliyoongozwa na Askofu wa Jimbo hilo Christopher Ndizeye. Amesema haki inapaswa kutendeka kuanzia ngazi ya familia pamoja na kusisitiza umoja wa watanzania kama jambo muhimu litakalopelekea maendeleo ya haraka.
Aidha amewahimiza wananchi kutumia mvua zinazoendelea kunyeesha nchini katika kupanda miti pamoja na kuongeza jitihada katika kujali mazingira ambayo yameharibiwa kwa kiasi kikubwa.
Pia Makamu wa Rais ametoa wito kwa viongozi wa dini na waumini kuendelea kuwaombea viongozi wa kitaifa ili waweze kupata hekima ya Mungu na kuwatendea watanzania haki ikiwa ni pamoja na kuwafikishia maendeleo wanayostahili.
Makamu wa Rais anaendelea na ziara ya kikazi mkoani Shinyanga ambapo anatarajia kuweka jiwe la msingi mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) Isaka – Tabora kilometa 165, kuweka jiwe la msingi hospitali ya Rufaa Shinyanga , kuweka jiwe la msingi ujenzi wa mradi wa maji tinde pamoja na kuzungumza na wananchi wa mkoa huo.s