Na Mwandishi Wetu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Dar es Salaam
Ikiwa zimepita takribani siku 18 tangu kumalizika na kuanza kwa mwaka 2023,Baraza la Taifa la Usalama barabarani likiongozwa na Mwenyekiti wake Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Jumanne Sagini limekutana mapema Leo na kufanya tathmini ya hali ya usalama barabarani kwa kipindi Chote Cha sikukuu ambapo matukio ya ajali za barabarani na vifo yalipungua kwa kiasi kikubwa.
Akizungumza mara baada ya kumaliza kwa kikao Kazi Cha baraza la Taifa la Usalama barabarani Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na Mwenyekiti wa Baraza hilo amesema kuwa jitihada kubwa zilizofanywa na kikosi Cha usalama barabarani na pia Wananchi wanaotumia Vyombo vya usafiri kusimamia sheria zimepelekea matukio ya ajali za barabarani kuendelea kupungua.
“Niwapongeze Wanachi ambao mlikuwa mnatumia vyombo vya moto kufanya safari kutoka maeneo mbalimbali Nchi , kwa kuzingatia sheria za Usalama barabarani kwa kipindi Chote Cha sikukuu.”
Aliendelea”Pia niwapongeze askari wa Usalama barabarani,jeshi la polisi na Vyombo vingine vya usalama na kusimamia sheria za kudhibiti matukio yoyote ya uhalifu”Alisema Sagini
Ramadhan Nganzi Kamishna msaidizi wa jeshi la polisi na Kamanda wa kikosi Cha usalama barabarani amesema miongoni mwa mapendekezo yaliyotolewa na baraza ni pamoja na kutolewa elimu zaidi na usimamizi wa karibu kwa makundi ya waendesha bodaboda kwani wengi wao ni Vijana ambao wanapoteza maisha na pia wakati mwingine kuwasababishia ulemavu wa kudumu.
Katika hatua nyingine mjumbe wa baraza hilo amesema baraza Hilo pia limekuja na mapendekezo ya namna ya kutafuta vyanzo vya mapato vitakavyowezesha kikosi Cha Usalama barabarani katika kutekeleza Majukumu yao.