Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui akizungumza machache katika ufunguzi wa mkutano kwa madakati uliofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Madinat Albahr Chukwani.
Mjumbe wa ZOP Dkt Naufal Kassim akitoa maelezo mafupi kuhusu mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Madinat Albahr Chukwani nje kidogo ya Mji wa Zanzibar
Waziri wa Afya Nassor Ahmed Mazrui akipokea zawadi kutoka kwa Rais wa Taasisi ya Oman Canser Assosition Dkt Wahid Ali Sayyid ghafla iliyofanyika katika Ukumbi wa Madinat Albahr Chukwani.
Baadhi ya wajumbe kutoka Taasisi ya Oman Canser Assosition wakisikiliza kwa makini maelezo yanayotolewa na Waziri wa Afya ambae hayupo pichani katika ghafla ya ufunguzi wa mkutano huo uliyofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Madinat Albahr.
………………………….
Na Rahma Khamis -Maelezo
Waziri wa Afya Zanziba Mh, Nassor Ahmed Mazrui ameitaka jamii kufika Hospitali mapema mara tu wanapojigundua na mabadiliko katika mwili ili kujikinga na maradhi ya saratani.
Ameyasema hayo katika Ukumbi wa Hoteli ya Madinat Albahr Chukwani nje kidgo ya Mji wa Zanzibar wakati alipokua akifungua mkutano wa mafunzo ya Tiba Shufaa kwa madaktari (Parliative Care).
Amesema maradhi hayo ni janga la Dunia kutokana na kuongezeka kwa kasi siku hadi siku hivyo kutolewa kwa mafunzo hayo itasaidia jamii kufahamu athari za maradhi hayo na kujikinga.
Aidha amefahamisha kuwa maradhi hayo yanaathiri sana jamii hivyo ni jabo muhimu kwa madakatari kupatiwa mafunzo kutokana na maradhi hayo yanaweza kumpata mtu yeyote.
Waziri Mazrui ameeleza katika kuhakikisha maradhi hayo yanapatiwa tiba sahihi wanatarajia kuboresha zaidi kitengo cha Saratani Hospitali ya Mnazimmoja kwa kuweka vifaa vya kisasa na madaktari waliobobea ili kuwaondeshea maumivu wagonjwa.
Hata hivyo Waziri huyo amesema kuwa iwapo wananchi watafanya uchunguzi wa afya zao na kujigundua kuwa hawana tatizo hilo kinga ipo hasa kwa saratani ya shingo ya kizazi.
Nae Mjumbe kutoka ( ZOP) ambae pia ni Katibu Mtendaji wa Taasis ya Oman Censa Assossition Zanibar Dkt, Naufal Kassim amesema kuwa mafunzo hayo ni muhimu ktokana kua maradhi hayo yanatibika iwapo mgonjwa atajigundua mapema na kupata matibabu.
Aidha amefahamisha kuwa lengo la mafunzo hayo kuhakisha mgonjwa anaeumwa na maradhi hayo anakuwa na ugonjwa huo lakini hateseki wala hayamsumbui na anaishi kwa matumaini bila ya wasiwasi wowote.
Dkt Naufal ameiasa jamii kuacha kula vyakula visivyo vya asili na badala yake kutumia vyakula vya asili ili kujikinga na maradhi hayo.
Kwa upande wake Daktari Nooren Abdughafoor wa Kitengo cha Dharura Hospitali ya Mnazimmoja amesema kuwa baada ya kumaliza mafunzo ya Advance wanatarajia kufika katika kitengo cha saratani hospitani hapo na kuwaona wagonjwa ambao wanahitaji uangalifu zaidi ili kuwasaidia.
Aidha amefahamisha kuwa mafunzo hayo ni muendelezo kwani awali walipatiwa mafunzo kama hayo ambayo ni foundation na badae kukaa na waumini wa dini zote kuwapa elimu kuhusu maradhi hayo.
Mafunzo hayo ni ya siku saba na yameandaliwa na Taasisi ya Maradhi ya Saratani Oman (OMAN CANSER ASSOSITION) kwa kushirikiana na Haospiati ya Mnazimmoja.