***********
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM), Taifa Bw. Fadhil Maganya ameipongeza Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Dar es Salaam kwa kuandaa Mafunzo kwa Viongozi wa kamati ya Utekelezaji katika kuimarisha utendaji kazi.
Ametoa pongezi hizo Januari 13,2023 Kigamboni Jijini Dar es Salaam wakati alipotembelea eneo ambalo Mafunzo hayo yanaendelea kutolewa kwa viongozi wa Kamati ya Utekelezaji.
Aidha Bw.Maganya amewataka viongozi hao kuwa na upendo na kushirikiana katika kuijenga na kuiimarisha Jumuiya na kuondoa tofauti zao pindi zinapotokea.
“Tukianza kukwaruzana kwaruzana,hatutakwenda,tushikamane, letu liwe moja na tuoneshe tofauti na Jumuiya zingine , utofauti uwe chanya usiwe utofauti wa kugongana gongana ,Kamati za utekelezaji mshikamane na uongozi wenu ufane”. Amesema
Amesema Dar es Salaam lazima iendelee kubaki ya kuigwa kwa hivyo anashukuru kwa fursa hiyo wao hawajatengeneza baraza na wala hawana Kamati ya utekelezaji na kamati zingine ndogo ndogo kwasababu alitaka wapate muda kufahamiana vizuri pia .
Katika hatua nyingine Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM, Taifa Bw. Fadhil Maganya ameipa heshima Jumuiya ya Wazazi mkoa wa Dar es Salaam kujipanga kwa pamoja katika maandalizi makubwa ya kuzindua kongamano la malezi la Jumuiya ya hiyo mapema mwaka huu, litakaloenda nchini nzima,na kwamba ameiomba mikoa mingine kuiga mfano wa mkoa wa Dar es Salaam kwa kuanza mafunzo ya uongozi kwa uharaka.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Dar es Salam, Bi.Khadija Ally amesema dhumuni la mafunzo hayo ni kuhakikisha wanatengeneza viongozi sahihi katika nyakati sahihi ili waweze kuongoza Jumuiya na Chama cha Mapinduzi nchini.
Pamoja na hayo Bi.Khadija amesema kuwa katika kuelekea kwenye Uchaguzi 2024 pamoja na 2025 dhumuni la Jumuiya na Chama kwa ujumla ni kuhakikisha wanapata ushindi kwa kishindo.
“Ushindi wa kishindo ambao tunaenda kuupata lazima tuwe na viongozi makini ambao wanakisi sifa na weledi katika Chama cha mapinduzi kwahiyo wametekeleza azimio la Mkutano Mkuu wa Kumi kwa kutoa Mafunzo kwa vitendo na tumeanza na Mkoa wa Dar es Salaam”. Amesema
Hata hivyo amemuhakikishia Mwenyekiti kwamba Mkoa wa Dar es Salaam uko tayari kushirikiana nae bega kwa bega na kuhakikisha dira yake ya Jumuiya ya Wazazi inang’ara na kuisimamia vyema Ilani ya Chama cha Mapinduzi ndani ya Mkoa huo na taifa kwa Ujumla.