Daktari wa Binywa wa Magonjwa ya Ndani Hospitali ya Taifa Muhimbili Mloganzila akimfanyia uchunguzi Mwananchi aliyekuja kupata huduma ya uchunguzi na matibabu ya moyo katika kambi hiyo iliyodumu kwa muda wa siku nne Baadhi ya wananchi wakisubiri kupata huduma Wataalamu wakiendelea kutoa huduma kwa wananchi waliofika kupatiwa kufanyiwa uchunguzi na kupatiwa matibabu Daktari Bingwa wa Macho Hospitali ya Taifa Muhimbili Mloganzila Dkt. Yusta Mtogo akimfanyia uchunguzi mwananchi aliyekuja kupata huduma ya macho. Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala Dkt. Zavery Benela akiwa katika picha ya pamoja na wataalamu walioshiriki katika zoezi la kutoa huduma na kufanya uchunguzi katika kambi hiyo.
*******************
Wananchi 710 wamenufaika na huduma za uchunguzi na matibabu kupitia kambi maalumu iliyoendeshwa na Madaktari Bingwa wa Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila kwa kushirikiana na Madaktari wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala kwa muda siku nne.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji Hospitali ya Taifa Muhimbili, Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Shirikisha Dkt. Lulu Sakafu amesema kuwa lengo kambi ilikuwa ni kuwajengea uwezo wataalamu wa Hospitali ya Mwananyamala pamoja na kusogezea huduma za kibingwa na za kibobezi kwa wananchi waliopo mwananyamala na maeneo ya jirani.
“Lengo la Hospitali ya Taifa Muhimbili Mloganzila limefanikiwa kwa kiwango kikubwa, tunashukuru kambi ilienda vizuri ambapo wataalamu wetu wameshirikiana bega kwa bega na wataalamu wa mwananyamala katika kutoa huduma jambo ambalo limejenga ushirikiano endelevu” ameeleza Dkt. Sakafu
Aidha Dkt. Sakafu ametoa wito kwa wananchi kujiunga na bima ya afya kwa kuwa huduma za kibingwa ni ghali na si rahisi kwa wananchi wa kawaida kuzimudu kumudu kwa fedha taslimu.
Kwa upande wake Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala Dkt. Aileen Barongo amesema kuwa muitikio wa wananchi umekuwa mkubwa
muitikio umekuwa mkubwa na wananchi wengi wamejitokeza kufanyiwa uchunguzi na kwa waliokutwa na matatizo wamepatiwa matibabu.
“Tumefanya uchunguzi kwa muda wa siku nne na mpaka sasa wananchi 710 wamefanyiwa uchunguzi, idara ambayo imepata wagonjwa wengi ni Idara ya Macho, ambapo wameona wagonjwa 270 wenye matatizo mbalimbali ya macho” ameelez Dkt. Barongo.
Kwa upande wake mmoja wa wananchi wa Mwananyamala Bi. Rahma Sharifu ambaye amefanyiwa uchunguzi na kupata elimu amewashukuru sana wataalamu wa Muhimbili-Mloganzila na Mwananyamala kwa kuwa kambi hiyo imenufaisha
Kambi hiyo imefanyika katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwanayamala ilianza Januari 9 na kuhitimishwa Januari 13,2023. Huduma zilizotolewa ni uchunguzi wa magonjwa ya mfumo wa mkojo, mifupa, macho, kisukari pamoja na moyo.