***********************
Mkuu wa wilaya ya Ikungi Mhe. Jerry C. Muro pamoja na viongozi wa kata ya Irisya wakiongozwa na mwenyekiti wa halmashauri ya ikungi Mhe. Ali juma mwanga ambae ni diwani wa irisya wamefanikiwa kuumaliza mgogoro wa ardhi baina ya Mama Hadija Mohamed na Ndugu Masoud Jumanne Tipa wa kitongoji cha mghondwe kijiji cha munyu kata ya irisya
Mgogoro huo uliodumu kwa miaka 18 mara baada ya kumalizika kwenye baraza la ardhi kata na wilaya lakini bado wananchi hao waliendelea kuvutana hatua iliyosababisha eneo kutolimwa katika msimu huu wa kilimo hatua ambayo Mkuu wa wilaya Mhe. Muro amesema haipaswi kuendelea kuachwa mana lazima ardhi ilimwe wananchi waondokane na umasikini
Akizungumza mara baada ya kutembelea shamba hilo na kukagua nyaraka za umiliki na kufuatilia mwenendo wa shauri hilo katika mabaraza ya ardhi Mhe. Muro amebaini Mama Hadija Mohamed ambae ni mjane ana nyaraka zote muhimu za umiliki ikiwemo hati ya makazi ya kimila na nyaraka alizonunua shamba hilo kutoka kwa Marehemu Robert mikindo ambae alipewa shamba hilo na baba mzazi wa Masoud Jumanne mtipa ambae yeye ameendelea kulalamikan kuwa eneo hilo ni la urithi wakati baba yao alishalitoa kwa marehemu Robert mikindo ambae alimuuzia mama Hadija mohamed ambae amekuwa akilitumia shamba hilo kwa miaka zaidi ya 15
Awali mwenyekiti wa halmashauri ya ikungi ambae ni diwani wa kata ya irisya amesema kumalizika kwa mgogoro huo kutatoa nafasi ya kuendelea kwa shughuli za kilimo katika msimu huu wa kilimo hatua itakayomsaidia mama mjane kujikimu kimaisha na familia yake